Vita vya Yemen ni vita dhidi ya watoto
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45148-vita_vya_yemen_ni_vita_dhidi_ya_watoto
Baada ya kutembelea, Sanaa, mji mkuu wa Yemen na maeneo mengine ya kusini mwa nchi hiyo, Susanna Kruger mkuu wa mfuko wa watoto wa Save the Children, umaitaja hali ya nchi hiyo kuwa ya kusikitisha na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 30, 2018 02:33 UTC
  • Vita vya Yemen ni vita dhidi ya watoto

Baada ya kutembelea, Sanaa, mji mkuu wa Yemen na maeneo mengine ya kusini mwa nchi hiyo, Susanna Kruger mkuu wa mfuko wa watoto wa Save the Children, umaitaja hali ya nchi hiyo kuwa ya kusikitisha na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani.

Kruger amesema mauaji ya kiholela, magonjwa na baa la njaa linalowakabili maelfu ya watu wa nchi hiyo, yote hayo yanatokana na hujuma ya mabomu ambayo yamekuwa yakidondoshwa nchini humo na Saudi Arabia na washirika wake na kusisitiza juu ya udharura wa Umoja wa Matifa kuingilia kati kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia Wayemen wanaoendelea kuteseka. Kuhusiana na suala hilo, hivi karibuni gazeti la Irish Times linalochapishwa mjini Dublin liliashiria maneno ya maafisa wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya kibinadamu ya kutisha inayoshuhudiwa huko Yemen na kuandika kuwa vita vya Yemen kwa hakika ni vita dhidi ya watoto wa nchi hiyo. Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanasema kwama mauaji ya umati kama yale yanayoendelea kutekelezwa na Saudia huko Yemen na hasa dhidi ya watoto, ni aina mbaya zaidi ya ugaidi.

Hospotali za Yemen hazina uwezo wa kukabiliana na wahanga wa uchokozi wa Saudia

Kuendelea kutolewa tahadhari za mashirika ya kimataifa kuhusiana na hali mbaya ya Yemen kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya Saudia nchini humo kwa hakika kunabainisha wazi ukubwa wa mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo masikini ya Kiarabu. Kufuatia ishara ya Marekani, Saudia ilianzisha hujuma kubwa ya kijeshi dhidi ya Yemen mnamo tarehe 26 Machi 2015 ambapo mbali na kuharibiwa miundombinu muhimu ya nchi hiyo yakiwemo mashule na mahospitali, zaidi ya Wayemen elfu 12 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa bila hatia yoyote. Kwa kushadidisha mauaji hayo dhidi ya watoto wa Yemen, Saudia inataka kuwatia hofu na woga watu wa nchi hiyo ili wasalimu amri mbele ya matakwa yake ya kujitanua katika nchi hiyo. Bika shaka jambo ambalo limeshajiisha na kudumisha jinai za Saudia huko Yemen na hasa mauaji ya watoto wadogo wasio na hatia, ni kimya na uzembe wa viongozi wa Umoja wa Mataifa mbele ya jinai hizo. Kutokana na siasa zake za mgangano ambapo kwa upande mmoja unalaani jinai hizo na kwa upande wa pili kutochukua hatua yoyote ya maana ya kukabiliana na jinai hizo, Umoja wa Mataifa umeshindwa kabisa kuzuia kuendelea kwa jinai hizo za Saudi na washirika wake nchini Yemen.

Sehemu ya jinai zinazotekelezwa na Saudia katika makazi ya raia wa Yemen

Nukta muhimu hapa ni kwamba kwa kueneza jinai zake nchini Yemen Saudia imedhiri kuwa mfano wa wazi kabisa wa watenda jinai za kivita. Licha ya jinai hizo za kutisha lakini hivi karibuni Saudia, kupitia uungaji mkono wa nchi za Magharibi, ilichaguliwa tena kuwa mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Kuzembea Umoja huo katika kukabiliana na jinai za Saudia kumeishajiisha nchi hiyo kudumisha jinai zake dhidi ya watu wa Yemen na hivyo kuwafanya walimwengu waendelee kushuhudia kuharibika zaidi kwa mgogoro wa kibinadamu nchini humo. Hii ni katika hali ambayo umoja huo unaweza kuwashtaki watawala wa Aal Saud kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuhusiana na jinai hizo kupitia Baraza la Usalama au Katibu Mkuu wake. Hivyo hatua ya Baraza la Usalama ya kupuuza mgogoro wa kibinadamu wa Yemen imeiruhusu Saudia kuendelea kupuuza maazimio na sheria za kimataifa na hivyo kushadidisha jinai zake dhidi ya watu wa Yemen.

Baadhi ya askari wa Sudan wanaoshirikiana na Saudia dhidi ya watu wa Yemen

Hii ni katika hali ambayo jinai hizo sasa zinatekelezwa kwa namna ya kutisha dhidi ya Wayemen wasio na ulinzi ili kufunika aibu ya watawala wa Saudia ambao licha ya kuwa na silaha za kisasa kabisa na kushirikiana na nchi kadhaa katika jinai hizo, lakini wameshindwa kabisa kufikia malengo yao nchini humo. Sisitizo la watawala hao la kuendeleza vita vya kichokozi dhidi ya Yemen bila shaka limeibana zaidi nchi hiyo na hivyo kuzidisha maafa ya kibadamu nchini humo.