Ushindi wa Palestina; utukufu wa ulimwengu wa Kiislamu
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistatijia cha Taasisi ya Kimataifa ya Mweamko wa Kiislamu amesema kwamba ushindi wa taifa la Palestina dhidi ya utawala haramu wa Isreal unauletea utukufu ulimwengu wa Kiislamu.
Akizungumza jana usiku hapa mjini Tehran katika kongamano la wanaharakati na watetezi wa taifa la Palestina, Hussein Akbari amesema kwamba kama isingekuwa Palestina, jinai za mfumo wa uistikabari duniani dhidi ya Waislamu hazingewekwa wazi na kwamba kama yasingekuwa ni Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, malengo ya utawala ghasibu wa Israel yangefikiwa kirahisi na hivyo kupotea kabisa kwa athari na utambulisho wa Palestina. Akbari ameendelea kusema kwamba utawala wa Kizayuni na Marekani haziko tena katika hali na mazingira mazuri ya huko nyumba na kwamba zimepoteza uungaji mkono wao katika eneo la Mashariki ya Kati ambapo pia taifa la Palestina limefikia natija hii kwamba njia bora na ya pekee ya kukabiliana na utawala wa kijinai wa Israel ni kupambana nao moja kwa moja bila kuhadaika na mapatano yasiyotekelezwa na utawala huo.
Ameendelea kusema kuwa hii leo ulimwengu wa uistikbari unatambua vyema kwamba iwapo utautishia mrengo wa mapambano ya Kiislamu bila shaka utakabiliwa na jibu kali kwa sababu leo mrengo huo una nguvu kubwa ambayo itausambaratisha mora moja utawala haramu wa Israel iwapo utafanya kosa la kutaka kuuhujumu. Akizungumza katika kongamano hilo Khalid Quddumi, mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS hapa mjini Tehran amesema kuwa Wazayuni hawafahamu lugha nyingine isipokuwa ya kutekeleza jinai na mauaji dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na kwamba bila shaka damu ya mashahidi wa Kipalestina inayoendelea kumwagwa na utawala huo ghasibu hatimaye itakuwa na athari kubwa dhidi ya utawala huo wa Kizayuni.