Silaha za Israel zakutwa katika maeneo yaliyokombolewa huko Daraa, Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46439-silaha_za_israel_zakutwa_katika_maeneo_yaliyokombolewa_huko_daraa_syria
Jeshi la Syria limenasa maghala kadhaa ya silaha na zana za kivita ambazo baadhi yake zimeundwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jun 29, 2018 10:43 UTC
  • Silaha za Israel zakutwa katika maeneo yaliyokombolewa huko Daraa, Syria

Jeshi la Syria limenasa maghala kadhaa ya silaha na zana za kivita ambazo baadhi yake zimeundwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Silaha hizo zimenaswa katika oparesheni ya kukusanya silaha iliyofanyika katika vitongoji viwili vilivyokombolewa hivi karibuni huko Syria vya Busr al Harir na Nahta huko mashariki mwa mkoa wa Daraa kusini mwa nchi hiyo. 

Maghala hayo ya silaha yamekutwa na mabomu, RPG na bunduki za rashasha, makombora, maguruneti na silaha nyinginezo. Jeshi la Syria linayatumia maneo yaliyokombolewa kama vituo vya kuendesha mapambano dhidi ya magaidi.  

Kukombolewa kwa vitongoji hivyo ni mafanikio makubwa kwa jeshi la Syria kwa sababu maeneo hayo yanahesabiwa kuwa vituo vikuu vya makundi ya kigaidi katika mpaka wa Jordan na eneo la Al Laja ambalo limekuwa likitumia kuwafikishia misaada magaidi wa Kiwahabi. 

Aidha  wakimbizi karibu 500 wa Syria wamerejea nyumbani baada ya kuwa nje kwa miaka mitano baada ya kufurushwa kikamilifu magaidi huko Al Qalamou, Syria.  

Wakimbizi wa Syria wakirejea nyumbani