Ansarullah: Madai ya Imarati ya kusimamisha hujuma zake Hudaydah ni urongo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46508-ansarullah_madai_ya_imarati_ya_kusimamisha_hujuma_zake_hudaydah_ni_urongo
Harakati ya Ansarullah ya Yemen imekadhibisha madai yaliyotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu kwamba eti imesitisha oparesheni ya kutaka kukalia kwa mabavu mji wa bandari wa al-Hudaydah nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 02, 2018 07:00 UTC
  • Ansarullah: Madai ya Imarati ya kusimamisha hujuma zake Hudaydah ni urongo

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imekadhibisha madai yaliyotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu kwamba eti imesitisha oparesheni ya kutaka kukalia kwa mabavu mji wa bandari wa al-Hudaydah nchini Yemen.

Mohammed Abdul-Salam, msemaji wa Ansarullah amesema madai hayo ya Imarati ni urongo mtupu na yametolewa kwa lengo la kupotosha fikra za walio wengi.

Abdul-Salam aliyasema hayo jana Jumapili katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya lugha ya Kiarabu ya harakati hiyo na kubainisha kuwa, UAE ingali inaendeleza uvamizi na hujuma zake dhidi ya mji huo wa kistratajia.

Hapo jana Anwar Gargash, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE  katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter alidai kuwa, Imarati imesitisha oparesheni za kijeshi katika mji huo kwa lengo la kurahisisha kazi za Martin Griffiths, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ili kuweza kupatikana mapatano ya kuondoka bila masharti wapiganaji wa Ansarullah katika mji wa Al Hudaydah na bandari ya mji huo. 

Raia wa Yemen wakikimbia mji wa Hudaydah

Mjumbe huyo wa UN hapo awali alikuwa ametangaza kuwa, kwa mujibu wa mipango iliyofanyika, pande zote katika mgogoro wa Yemen zitafika katika meza ya mazungumzo, huku akitahadahrisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu kutokana na kushadidi mashambulizi dhidi ya Bandari ya al Hudayday.

Wanajeshi vamizi katika muungano unaoongozwa na Saudia na unaopata himaya ya Marekani, Uingereza na Ufaransa, mnamo Juni 13 ulipuuza tahadahri ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuhatarishwa maisha ya raia mjini Al Hudayda na kuanzisha hujuma kali ya anga, nchi kavu na baharini dhidi ya eneo hilo.