Bahrain inazuia watu kumtembelea Sheikh Qassim hospitalini London
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46792-bahrain_inazuia_watu_kumtembelea_sheikh_qassim_hospitalini_london
Kiongozi wa chama kimoja cha upinzani cha Bahrain amesema watawala wa Manama wanazuia watu kwenda kumtembelea Sheikh Isa Qassim hospitalini mjini London nchini Uingereza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2018 02:55 UTC
  • Bahrain inazuia watu kumtembelea Sheikh Qassim hospitalini London

Kiongozi wa chama kimoja cha upinzani cha Bahrain amesema watawala wa Manama wanazuia watu kwenda kumtembelea Sheikh Isa Qassim hospitalini mjini London nchini Uingereza.

Saeed al-Shehabi, kinara wa chama cha Bahraini Freedom Movement chenye makao yake mjini London amesema watu wamezuiwa kumuona mwanazuoni na kiongozi huyo mkubwa wa mwamko wa wananchi wa Bahrain, na hakuna mtu yeyote anayejua kuhusu hali yake ya kiafya.

Amesema, "hakuna anayejua kuhusu mchakato wa matibabu ya msomi huyo wa Kiislamu, inaonekana amepelekwa katika hospitali tofauti na ile ambayo madaktari walishauri apelekwe mjini London."

Maandamano ya Wabahrain ya kumuunga mkono Skh. Qassim 

Baada ya hali ya Sheikh Isa Qassim kuwa mbaya na kadhalika kushtadi malalamiko ya wananchi katika kulaani kifungo cha nyumbani dhidi ya mwanazuoni huyo, Julai 6 Hamad bin Isa Al Khalifa, Mfalme wa Bahrain alilazimika kutoa amri na chini ya uangalizi wa madaktari, kupelekwa nje ya nchi mwanazuoni huyo kwa ajili ya kupata matibabu. 

Sheikh Isa Qassim ambaye watawala wa Manama walimpokonya uraia wake mwaka 2016, amekuwa akiishi chini ya ulinzi mkali katika kifungo cha nyumbani mjini Derna, kwa zaidi ya siku 400, licha ya kuzorota hali yake ya kiafya.