Mufti wa Quds atahadharisdha kuhusu hali mbaya ya Msikiti wa Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46886-mufti_wa_quds_atahadharisdha_kuhusu_hali_mbaya_ya_msikiti_wa_quds
Mufti wa Msikiti mtakatifu wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya msikiti huo ambacho ndicho kibla cha kwanza cha Waislamu kote duniani.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Jul 19, 2018 16:59 UTC
  • Mufti wa Quds atahadharisdha kuhusu hali mbaya ya Msikiti wa Quds

Mufti wa Msikiti mtakatifu wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya msikiti huo ambacho ndicho kibla cha kwanza cha Waislamu kote duniani.

Sheikh Muhammad Hussein amesisitiza kuwa hali ya sasa ya Msikiti wa al Aqsa inatisha na kusema mashambulizi yanayofanywa kila siku dhidi ya msikiti huo na mashimo yanayochimbwa na utawala wa kizayuni wa Israel chini yake vinahatarisha majengo yake. 

Sheikh Muhammad Hussein amewataka viongozi wa Umma wa Kiislamu kuchukua hatua za dharura za kulinda eneo hilo takatifu.

Askari wa Israel wameuzingira Msikiti wa al Aqsa

Wakati huo huo zaidi ya walowezi 150 wa Kizayuni jana Jumatano walivamia na kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa na kuuvunjia heshima. Baada ya hujuma hiyo, Sheikh Ikrima Sabri ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kiislamu ya Baitul Muqaddas na hatibu mkuu wa Msikiti wa al Aqsa amesema kuwa shambulizi hilo la walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa ni jinai na kitendo kinachovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Mamia ya walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakiingia katika Msikiti wa al Aqsa kila siku na wakati huo askari wa utawala wa Israel wamekuwa wakifunga eneo hilo na kuwazuia Waislamu kufanya ibada zao.