Maandamano Bahrain kutangaza mshikamano na Sheikh Isa Qassim
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46905-maandamano_bahrain_kutangaza_mshikamano_na_sheikh_isa_qassim
Wananchi wa Bahrain leo wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu, Manama, kuonyesha mshikamano wao na mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Sheikh Isa Qassim anayepata matibabu nje ya nchi
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 20, 2018 09:43 UTC
  • Maandamano Bahrain kutangaza mshikamano na Sheikh Isa Qassim

Wananchi wa Bahrain leo wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu, Manama, kuonyesha mshikamano wao na mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Sheikh Isa Qassim anayepata matibabu nje ya nchi

Taarifa zinasema wananchi walioshiriki katika maandamano hayo wametangaza kuendelea kumuuunga mkono Sheikh Qassim ambaye amelazimika kupata matibabu nje ya nchi kutokana na mateso aliyoyapata mikononi mwa ufalme wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa ambao unatumia mkono wa chuma kuitawala nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Hali kadhalika waandamanaji wametangaza uungaji mkono wao kwa wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Aal Khalifa.

Sheikh Isa Qassim akitembelewa na wageni akiwa hospitalini

Sheikh Isa Qasseim ambaye ni mwanazuoni maarufu nchini Bahrain mnamo Julai 9 alielekea mjini London kupata matibabu ya dharura baada ya nyumba yake kuzingriwa kwa zaidi ya miaka miwili na wanajeshi wa ukoo wa Aal Khalifa.

Tangu tarehe 14 Februari mwaka 2011, Bahrain imekuwa ikishuhudia malalamiko ya wananchi wanaotaka utawala wa kidemokrasia lakini utawala wa nchi hiyo umeendelea kuwapuuza wananchi na badala yake kutumia mkono wa chuma na ukandamizaji mkubwa kuyazima.