Damascus yagundua hospitali ya Israel waliyojengewa magaidi kusini mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47638-damascus_yagundua_hospitali_ya_israel_waliyojengewa_magaidi_kusini_mwa_syria
Jeshi la Syria limegundua hospitali moja ya jangwani iliyokuwa inatumiwa na genge la kigaidi la Jabhat Fat'h al Sham ambalo zamani likuwa likijulikana kwa jina la Jab'hat al Nusra. Hospitali hiyo ambayo imejaa dawa na vifaa vilivyotengezwa Israel imegunduliwa katika mkoa wa Quneitra uliokombolewa hivi karibuni kusini mwa Syria.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Aug 23, 2018 10:36 UTC
  • Damascus yagundua hospitali ya Israel waliyojengewa magaidi kusini mwa Syria

Jeshi la Syria limegundua hospitali moja ya jangwani iliyokuwa inatumiwa na genge la kigaidi la Jabhat Fat'h al Sham ambalo zamani likuwa likijulikana kwa jina la Jab'hat al Nusra. Hospitali hiyo ambayo imejaa dawa na vifaa vilivyotengezwa Israel imegunduliwa katika mkoa wa Quneitra uliokombolewa hivi karibuni kusini mwa Syria.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo wamegundua hospitali hiyo katika kijiji cha al Rafid wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la kuusafisha mkoa wa Quneitra baada ya kuwafurusha magaidi.

Shirika hilo limesema kuwa, hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa kakama vile CT scans, X-ray, maabara na zana nyingine za kisasa ambazo zote walikuwa wamepatiwa magaidi hao na madola ya kigeni hususan utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakazi wa mkoa wa Quneitra wa kusini mwa Syria wakisherehekea ukombozi wa mkoa wao kutoka mikononi mwa magaidi wanaoungwa mkono na Israel na madola mengine ya kibeberu

 

Hospitali hiyo ina vyumba vya kufanya upasuaji vikiwa na zana zilizotengenezwa Israel kama ambavyo ina ghala iliyojaa madawa kutoka kwa utawala wa Kizayuni na Jordan. Vile vile katika hospitali hiyo vimepatikana vitu vingine vilivyotoka kwa nchi kadhaa za Ghuba ya Uajemi hususan Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati.

Julai 23 mwaka huu pia, wanajeshi wa Syria waligundua shehena kubwa ya madawa na vifaa vya tiba vilivyotengenezwa Israel katika hospitali nyingine ya jangwani iliyokuwa inatumiwa na magaidi wanaopata uungaji mkono wa madola ya kigeni katika mji wa Naba al Sakher.

Duru za kieneo ambazo hazikutaka kutajwa majina yao zimesema kuwa hospitali hiyo ya jangwa niilikuwa na vyumba kadhaa vya upasuaji, vifaa vya maabara na madawa; mbali na maghala yaliyokuwa yamejaa madawa kutoka Israel na Jordan.

Syria ilivamiwa na magenge ya kigaidi mwaka 2011 na siku zote serikali ya nchi hiyo inaishutumi Israel, nchi za Magharibi na vibaraka wao kwa kuyasaidia magenge ya kigaidi yanayofanya jinai ndani ya ardhi ya Syria.