Mgogoro wa mafuta kati ya Saudia na Kuwait waongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49341-mgogoro_wa_mafuta_kati_ya_saudia_na_kuwait_waongezeka
Mkuu wa Shirika la Mafuta la Kuwait, Nizar Mohammed Al-Adsani ameelezea habari ya kuendelea mogoro kati ya nchi hiyo na Saudi Arabia kuhusiana na maeneo yenye utajiri wa mafuta ya Wafra na Al-Khafji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 07, 2018 03:44 UTC
  • Mgogoro wa mafuta kati ya Saudia na Kuwait waongezeka

Mkuu wa Shirika la Mafuta la Kuwait, Nizar Mohammed Al-Adsani ameelezea habari ya kuendelea mogoro kati ya nchi hiyo na Saudi Arabia kuhusiana na maeneo yenye utajiri wa mafuta ya Wafra na Al-Khafji.

Al-Adsani ameyasema hayo katika kongamano la saba la kila mwaka la sekta ya mafuta nchini Kuwait na kuongeza kwamba, makubaliano kuhusiana na maeneo ya pamoja ya mafuta kati ya nchi mbili tayari yamekwisharatibiwa lakini utekelezwaji wake umefeli kutokana na kuwepo masuala ya kisiasa katika faili hilo badala ya masuala ya kiufundi. Kadhalika Mkuu wa Shirika la Mafuta la Kuwait amesema kuwa, safari ya Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia nchini Kuwait mwishoni mwa mwezi Septemba uliopita, haikuwa na matokeo yaliyotarajiwa.

Mkuu wa Shirika la Mafuta la Kuwait, Nizar Mohammed Al-Adsani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi kuu ya ufalme nchini Kuwait baada ya kumalizika kwa safari hiyo, Bin Salman alitaka kuimarishwa uhusiano wa kihistoria kati ya nchi mbili. Hii ni katika hali ambayo televisheni ya taifa nchini Kuwait mwishoni mwa safari ya mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia iliitaja safari hiyo kuwa chanya kwa ajili ya nchi hizo.