Az-Zahar: Muqawama utaendelea mpaka utawala wa Kizayuni uangamizwe kikamilifu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50372-az_zahar_muqawama_utaendelea_mpaka_utawala_wa_kizayuni_uangamizwe_kikamilifu
Mkuu wa mrengo wa Muqawama katika Bunge la Palestina, ameashiria mchango na nafasi ya Palestina katika mhimili wa Muqawama na kusisitiza kwamba: Inapasa uwepo uratibu kati ya muqawama wa Palestina, Syria na Lebanon ili kuangamizwa kwa Israel kuthibiti kikamilifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 23, 2018 23:19 UTC
  • Az-Zahar: Muqawama utaendelea mpaka utawala wa Kizayuni uangamizwe kikamilifu

Mkuu wa mrengo wa Muqawama katika Bunge la Palestina, ameashiria mchango na nafasi ya Palestina katika mhimili wa Muqawama na kusisitiza kwamba: Inapasa uwepo uratibu kati ya muqawama wa Palestina, Syria na Lebanon ili kuangamizwa kwa Israel kuthibiti kikamilifu.

Mahmoud Az-Zahar, ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Habari ya hapa nchini, ambapo mbali na kusisitiza kwamba Quds ni mji mkuu wa Palestina amebainisha kuwa: Inapasa kusimama imara kukabiliana na uvamizi wa adui mzayuni; na kama vita vitatokea katika ardhi ya Palestina, bila ya shaka mshindi atakuwa ni vikosi vya muqawama.

Huku akiashiria kwamba mnamo siku za usoni itadhihirika ni nani wanaowasaliti Wapalestina, Az-Zahar amesema: Baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi zinataka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, lakini msimamo thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni maghasibu hao kuondoka katika ardhi ya Palestina.

Mkuu wa mrengo wa muqawama katika Bunge la Palestina ameashiria pia ahadi za Umoja wa Mataifa kwa wananchi wa Palestina na akasema: Umoja huo ni mshirika wa utawala wa Kizayuni, kwa sababu nyumba na hospitali katika Ukanda wa Gaza zimebomolewa kikamilifu kutokana na hujuma za Wazayuni; na hospitali zilizosalia katika eneo hilo zina uhaba mkubwa wa fueli, lakini Umoja wa Mataifa hauchukui hatua yoyote kutatua matatizo hayo.

Kuhusu hukumu iliyotolewa na mahakama ya katiba ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kulivunja bunge la Palestina, Dakta Mahmoud Az-Zahar amesema, uamuzi huo ni batili na akaongeza kuwa: Kuvunjwa bunge hilo kuna uhusiano na mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne.../