Dawa zilizotengenezwa Israel zakutwa mikononi mwa magaidi huko Syria
Idadi kubwa ya dawa, silaha na zana za kijeshi zilizoundwa katika utawala wa Kizayuni na kupewa magaidi zimenaswa wakati wa kuwafurusha magaidi hao huko kusini mwa Syria.
Dawa hizo mbalimbali pamoja na silaha na zana za kijeshi zilizotengenezwa Israel zimenaswa kutoka kwa magaidi karibu na eneo la Quneitra, kusini mwa Syria. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, utawala wa Kizayuni ulikuwa ukiwaunga mkono kwa hali na mali magaidi waliokuwa wamejizatiti katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Syria; na hata magaidi waliokuwa wakijeruhiwa walikuwa wakisafirishwa kwa ajili ya kupewa matibabu na Wazayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.
Israel imekuwa ikiratibu na kuwapa magaidi taarifa za kiitelijinsia na kijasusi kuhusiana na harakati za jeshi la Syria. Inawapa pia magaidi hao silaha mbalimbali za kisasa kama vile makombora aina ya Tau ya kulenga vifaru.
Mwanzoni mwa mwaka huu pia askari usalama wa Syria walikamata idadi kubwa ya silaha za Marekani na Israel mikononi mwa magaidi huko Rif-Dimashq. Silaha hizo ni pamoja na makumi ya maelfu ya bunduki, makombora, vifaa vya mawasiliano n.k, ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye maghala ya chini ya ardhi.
