Visa vya Wazayuni kuwagonga kwa gari Wapalestina kwa makusudi vyaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53627-visa_vya_wazayuni_kuwagonga_kwa_gari_wapalestina_kwa_makusudi_vyaongezeka
Mlowezi wa Kizayuni amemgonga kwa gari Mpalestina kwa makusudi na kumuua shahidi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
May 21, 2019 09:26 UTC
  • Visa vya Wazayuni kuwagonga kwa gari Wapalestina kwa makusudi vyaongezeka

Mlowezi wa Kizayuni amemgonga kwa gari Mpalestina kwa makusudi na kumuua shahidi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti habari hiyo na kumtaja Mpalestina aliyeuawa katika tukio hilo kuwa ni Abdul Hafiz Barham, aliyekuwa na umri wa miaka 45.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo limefanyika leo Jumanne katika mji wa Qalqilya mashariki mwa Ukingo wa Magharibi.

Habari zaidi zinasema kuwa, baada ya kugongwa na gari hilo la Mzayuni, Mpalestina huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Nablus, ambapo aliaga dunia muda mfupi baadaye kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata.

Mtoto wa Kipalestina, mhanga wa jinai hiyo ya Wazayuni kwa kutumia gari

Mwezi uliopita, mwalimu wa kike Mpalestina aliuawa katika tukio jingine la kugongwa na gari la Mzayuni kwa makusudi karibu na mji wa Baitulahm (Bethlehem).

Matukio haya ya Wazayuni kuwagonga kwa gari Wapalestina kwa makusudi yameongeza katika miaka ya hivi karibuni katika Ukiongo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, ambapo aghalabu ya visa hivyo vinakosa kuchunguzwa na utawala mtenda jinai wa Israel.