Kituo cha nyuklia cha Israel kimekiri kuvujisha mada za radioactive
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i54078-kituo_cha_nyuklia_cha_israel_kimekiri_kuvujisha_mada_za_radioactive
Kituo cha nyuklia cha Demona kwa mara ya kwanza kimekiri kuwa kwa miaka kadhaa kimekuwa kikivujisha mada za radiocative.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jun 12, 2019 21:33 UTC
  • Kituo cha nyuklia cha Israel kimekiri kuvujisha mada za radioactive

Kituo cha nyuklia cha Demona kwa mara ya kwanza kimekiri kuwa kwa miaka kadhaa kimekuwa kikivujisha mada za radiocative.

Taarifa za kuvuja kwa mada za radioactive kutoka kituo hicho cha nyujklia cha Demona mali ya Israel zimefichuka baada ya mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha nguvu za atomiki kutaka alipwe fidia kutokana na maradhi ya saratani aliyopata. Kwa mujibu wa redio ya utawala wa Kizayuni; wakurugenzi wa kituo hicho cha Demona wamekiri kuwa kimekuwa kikivujisha mada za radioactive baada ya mfanyakazi wake huyo kuwasilisha mashtaka mahakamani. Mwaka 2017 pia kamisheni ya nishati ya nyuklia ya Israel iliafiki kuwalipa fidia wafanyakazi wengine 168 wa kituo hicho cha nyuklia waliodhurika na kupatwa na maradhi ya saratani. 

Utawala wa Kizayuni ulianza kujenga kwa siri kituo cha Demona mwaka 1958 kwa kusaidiwa na Ufaransa; na  kuanza kufanya kazi mwaka 1963. Umri wa wastani wa vituo vya nguvu za nyuklia ni karibu miaka 40; na kwa msingi huo umri munasibu kwa kituo hicho ulimalizika mwaka 2003 na sasa kinapasa kusitisha shughuli zake, lakini utawala wa Kizayuni hadi sasa unapindisha na kukwamisha kufungwa kwake kwa visingizio mbalimbali. 

Kituo hicho cha Demona kimekuwa hatari pia kwa nchi za Kiarabu hata kabla ya kilivyo katika hali ya uchakavu wa hivi sasa. Aidha ufukiaji wa taka za nyuklia wa kituo hicho ambao umekuwa ukifanywa katika jangwa la Naqab umekuwa ukilalamikiwa pakubwa. Wakati huo huo iwapo mlipuko utatokea katika kituo hicho hatari yake itaathiri eneo kubwa  na kuzikumba nchi za Palestina, Jordan, Lebanon na baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi hadi Cyprus. 

Jangwa la Naqab