Waziri Mkuu wa Iraq aondoa sheria ya kutotoka nje
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56430-waziri_mkuu_wa_iraq_aondoa_sheria_ya_kutotoka_nje
Waziri Mkuu wa Iraq ametangaza kuondolewa sheria ya kutotoka nje ambayo ilikuwa imeanza kutekelezwa kufuatia maandamano na ghasia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 05, 2019 03:59 UTC
  • Waziri Mkuu wa Iraq aondoa sheria ya kutotoka nje

Waziri Mkuu wa Iraq ametangaza kuondolewa sheria ya kutotoka nje ambayo ilikuwa imeanza kutekelezwa kufuatia maandamano na ghasia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Adel Abdul Mahdi Waziri Mkuu wa Iraq ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu nchini humo, Ijumaa usiku alitoa amri ya kuondolewa amri ya kutotoka nje iliyokuwa imeanza kutekelezwa Alhamisi.

Adel Abul Mahdi aidha amewaahidi waandamanaji kuwa atajibu matakwa yao halali.

Ijumaa usiku pia kulifanyika kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa usalama Iraq chini ya uwenyekiti wa Adel Abdul Mahdi kwa lengo la kuchunguza matukio ya hivi karibuni nchini humo.

Baadhi ya maeneo ya Iraq ukiwemo mji mkuu, Baghdad, yalishuhudia maandamano makubwa katika siku za hivi karibuni ambapo wananchi wamekuwa wakilalmikia hali mbya ya huduma za umma, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali.

Utulivu warejea Baghdad baada ya maandamano

Hata hivyo maadui wa serikali ya Iraq walijipenyeza miongoni mwa waandamanaji na kuchochea ghasia na machafuko ambapo hadi sasa watu 48 wanaripotiwa kuaga dunia.

Ushahidi unaonyesho kuwa maandaano hayo ya hivi karibuni nchini Iraq hayakuibuliwa na wananchi wenyewe bali yalichochewa na maadui. Imedokezwa kuwa asilimi 79 ya jumbe zote za Twitter ambazo zimesambazwa kuhusu maandamano ya Iraq zilienezwa na watumizi wa Twitter walioko Saudi Arabia.