Mbunge wa Palestina: Utawala wa Kizayuni unaendelea kuiyahudisha Quds
Mbunge anayeuwakilisha mji wa Quds katika bunge la Palestina amesema kuwa utawala wa Kizayuni unaendelea kutekeleza mipango yake iliyoikusudia kwa malengo maalumu na inastafidi na kushughulishwa Umma wa Kiislamu na Kiarabu na masuala yake ya ndani ili kusogeza mbele mipango yake hiyo.
Ahmad Atuan amesema kuwa utawala wa Kizayuni unaamini kuwa hali ya mambo iliyopo sasa ni fursa nzuri kwake kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kuiyahudisha Quds. Atuan ameashiria namna wakazi wa Quds pekee wanavyokabiliana na kusimama kidete mbele ya mashambulizi na njama za adui Mzayuni dhidi ya Quds na kusisitiza kuwa raia hao wapo mstari wa mbele katika kuutetea na kuulinda mji huo mtukufu.
Mbunge anayeuwakilisha mji wa Quds katika bunge la Palestina amesisitiza pia udharura wa kukabiliana na chokochoko za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu na ujenzi wake wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Quds kupitia kushiriki kwa wingi katika msikiti wa al Aqsa.
Ahmad Atuan ameutolea wito Umma wa Kiislamu na Kiarabu kuwaunga mkono wakazi wa mji wa Quds na kuwaharakishia misaada.