Iraq yasema maafisa wa usalama hawajatumia silaha dhidi ya waandamanaji
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56873-iraq_yasema_maafisa_wa_usalama_hawajatumia_silaha_dhidi_ya_waandamanaji
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq amesema vikosi vya usalama nchini humo havijatumia silaha dhidi ya waandamanaji katika maandamano ya hivi karibuni nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 27, 2019 02:38 UTC
  • Iraq yasema maafisa wa usalama hawajatumia silaha dhidi ya waandamanaji

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq amesema vikosi vya usalama nchini humo havijatumia silaha dhidi ya waandamanaji katika maandamano ya hivi karibuni nchini humo.

Khalid al-Mahna Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq katika ripoti siku ya Jumamosi, amepongeza misimamo ya Ayatullah Sistani, Marjaa wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Iraq na nasasa zake zenye thamani na busara katika hotuba za Sala ya Ijumaa. Ameongeza kuwa, katiba ya Iraq inawapa wananchi haki ya maandamano ya amani na inadhamini kulindwa maisha ya raia na mali za umma.

Waziri Mkuu wa Iraq Adel al Mahdi

Al-Mahna amekosoa namna ambavyo maandamano ya wananchi yametekwa na baadhi ya watu ambao wamepelekea yapoteze muelekeo wake sahihi. Aidha amesema idadi kadhaa ya maafisa wa usalama Iraq wameuawa au kujeruhiwa kutokana na maandamano ya wananchi kutumiwa vibaya.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq hali kadhalika amelaani vitendo vya kuteketeza moto idara za serikali na nyumba za raia na kusema, wale wote waliohusika katika vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali.