Twitter yafunga kurasa za Hizbullah na shirika la habari la Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57027-twitter_yafunga_kurasa_za_hizbullah_na_shirika_la_habari_la_quds
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imekosoa vikali hatua ya shirika la mtandao wa kijamii wa Twitter la Marekani ya kufuta kurasa zenye mfungamano na harakati hiyo kwenye mtandao huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2019 04:45 UTC
  • Twitter yafunga kurasa za Hizbullah na shirika la habari la Quds

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imekosoa vikali hatua ya shirika la mtandao wa kijamii wa Twitter la Marekani ya kufuta kurasa zenye mfungamano na harakati hiyo kwenye mtandao huo.

Kanali ya televisheni ya Al Manar inayomilikiwa na Hizbullah imesema kitendo cha kampuni ya Twitter cha kufunga akaunti yake kimechukuliwa kutokana na mashinikizo ya kisiasa. 

Haya yanajiri siku chache baada ya wimbi la maandamano ya wananchi wa Lebanon kumshinikiza Waziri Mkuu, Saad Hariri kutangaza kujiuzulu, huku umaarufu wa Hizbullah ukikuwa kwa kasi kubwa sio tu nchini Lebanon, bali katika eneo kwa ujumla.

Miezi michache iliyopita, Twitter ilifunga akaunti za mashirika ya habari ya Iran

Wakati huo huo, Twitter imefunga kurasa za Mtandao wa Habari wa Quds, moja ya vyanzo vikuu vya habari za Palestina ambazo zimekuwa zikiakisi uporaji na ukaliaji mabavu wa ardhi za Wapalestina unaofanywa na utawala haramu wa Israel.

Wanaharakati wa Palestina wanasema kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii yenye makao makuu yake nchini Marekani imefunga kurasa 50 za Quds News Network kutokana na mashinikizo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA), inayodai kuwa kurasa hizo za habari zimekiuka sheria za mtandao katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.