Mgombea urais Algeria: Syria inabidi irejee Arab League
(last modified Tue, 12 Nov 2019 02:58:24 GMT )
Nov 12, 2019 02:58 UTC
  • Mgombea urais Algeria: Syria inabidi irejee Arab League

Abdel Qadir bin Qrina, mgombea urais katika uchaguzi ujao wa Algeria amesema kuwa iwapo atashinda uchaguzi huo, basi atafanya juhudi kuhakikisha Syria inarudi kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League).

Ibin Qrina mkuu wa Harakati ya Kujenga Taifa ya Algeria na ambaye pia ni mmoja wa wagombea kwenye uchaguzi wa rais ujao nchini humo amesema kuwa, serikali ya Algiers haikukubali kitendo cha nchi za Kiarabu kukata uhusiano wao na Syria. Abdel Qadir bin Qrina amezidi kufafanua kuwa, kwa kipindi chote cha historia Damascus imekuwa ikiiunga mkono Algeria dhidi ya mkoloni Mfaransa. Amesema kuwa, Syria ni moja ya nchi ambazo daima zimekuwa zikipinga kuwa chini ya ubeberu wa nchi za Magharibi katika eneo la Asia Magharibi.

Raia wa Syria na Algeria daima wamekuwa wakipendana

Mgombea huyo wa urais katika uchaguzi ujao wa Algeria amesisitiza kwamba daima serikali ya Algiers itasimama pamoja na Syria kwa lengo la kuiwezesha Damascus kuvuka kipindi hiki kigumu cha migogoro. Siku ya Jumamosi Tume ya uchaguzi ya Algeria iliwatangaza wagombea watano watakaochuana katika uchaguzi wa rais, ambao umepangwa kufanyika tarehe 12 Disemba mwaka huu.