Maandamano ya "Haki ya Kurejea" Palestina yataendelea mpaka yafikie malengo yake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57441-maandamano_ya_haki_ya_kurejea_palestina_yataendelea_mpaka_yafikie_malengo_yake
Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya maandamano ya "Haki ya Kurejea" amesisitiza kuwa, maandamano ya Wapalestina ya "Haki ya kurejea" ambayo hufanyika kila Ijumaa yataendelea hadi pale Wapalestina watakapofikia malengo yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 23, 2019 04:37 UTC
  • Maandamano ya

Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya maandamano ya "Haki ya Kurejea" amesisitiza kuwa, maandamano ya Wapalestina ya "Haki ya kurejea" ambayo hufanyika kila Ijumaa yataendelea hadi pale Wapalestina watakapofikia malengo yao.

Mahir Mazhar amekanusha habari za kuweko mpango wa kufanyika maandamano ya Haki ya Kurejea kila mwezi badala ya kila Ijumaa na kusisitiza kuwa, mpango wa maandamano hayo ya kila Ijumaa uko pale pale na kwamba, hakuna mabadiliko.

Aidha amesema kuwa, maandamano hayo ya Haki ya Kurejea jana Ijumaa yalifutwa kutokana na sababu maalumu za kiusalama.

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" ya kupigania Wapalestina kurejea katika ardhi za mababu zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel yalianza tarehe 30 Machi 2018 siku ambayo ilisadifiana na kumbukumbu ya "Siku ya Ardhi" huko Palestina. Maandamano hayo hufanyika kila Ijumaa katika mpaka wa Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Maandamano ya Wapalestina ya "Haki ya Kurejea"

Siku ya Ardhi inayoadhimishwa kila mwaka huko Palestina ni kumbukumbu ya uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuteka ardhi za Wapalestina tarehe 30 Machi 1976 na kuziingiza ardhi hizo katika maeneo mengine ya Wapalestina ambayo imekuwa ikiyakalia kwa mabavu tangu mwaka 1948.

Hadi leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuziyahudisha ardhi hizo na kufuta kabisa utambulisho wake wa Kiislamu-Kipalestina.