Naibu wa Abubakr al-Baghdadi atiwa mbaroni nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57664-naibu_wa_abubakr_al_baghdadi_atiwa_mbaroni_nchini_iraq
Vikosi vya usalama vya Iraq vimemtia mbaroni naibu wa Abubakr al-Baghdadi, kinara aliyeuawa wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) huko kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-25T11:30:13+00:00 )
Dec 04, 2019 04:00 UTC
  • Naibu wa Abubakr al-Baghdadi atiwa mbaroni nchini Iraq

Vikosi vya usalama vya Iraq vimemtia mbaroni naibu wa Abubakr al-Baghdadi, kinara aliyeuawa wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) huko kaskazini mwa nchi hiyo.

Kituo cha upashaji habari cha Idara kuu ya vikosi vya ulinzi vya Iraq kimetangaza kuwa, Abu Khaldun, naibu wa Abubakr al-Baghdadi, alitiwa nguvuni hapo jana na vikosi vya usalama na polisi ya mji wa al Huwaijah mkoani Kirkuk akiwa ndani ya nyumba moja ya fleti.

Mtendajinai huyo katili ambaye huko nyuma alikuwa kamanada mkuu wa magaidi katika mkoa wa Salahuddin, kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, alikuwa amejificha mkoani Kirkuk huku akitumia jina bandia la Shaalan Ubayd.

Magaidi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS)

Katika miaka ya karibuni, kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, chini ya uongozi wa Abubakr al-Baghdadi, lilivamia na kuyakalia kwa mabavu maeneo mengi ya ardhi za Iraq na Syria na kutenda jinai zisizohesabika kwa msaada na uungaji mkono wa fedha na silaha wa Marekani, Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kundi hilo la kigaidi, limefanya hujuma na mashambulio kadhaa ya kigaidi katika nchi zingine pia duniani zikiwemo za Ulaya, eneo la Asia Magharibi na barani Afrika.../