Uturuki: Hatukubaliani na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57905-uturuki_hatukubaliani_na_vikwazo_vya_marekani_dhidi_ya_iran
Serikali ya Uturuki kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo imekosoa vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 15, 2019 23:04 UTC
  • Uturuki: Hatukubaliani na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Serikali ya Uturuki kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo imekosoa vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki sambamba na kupinga vikwazo hivyo vya Marekani dhidi ya Iran amesema kuwa, vikwazo vya Washington vinawalenga wananchi wa Iran na si vinginevyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameongeza kwamba, vikwazo havijawahi kuwa na mafanikio kwa ajili ya White House na wala havitakuwa na maslahi yoyote hapo baadaye. Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei 2018 rais wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya upande mmoja ya kukiuka majukumu ya Washington ndani ya mapatano ya nyukli ya JCPOA, na akaiondoa nchi yake katika mapatano hayo ya kimataifa.

Iran na Uturuki ni nchi mbili jirani na ndugu za Kiislamu zenye uhusiano mzuri wa muda mrefu

Mbali na hayo Trump alitangaza kuirejeshea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vya nyuklia vilivyokuwa vimeondolewa baada ya kufikiwa mapatano hayo. Hatua hiyo iliyo kinyume cha sheria imeendelea kukabiliwa na upinzani mkubwa katika ngazi ya ndani na kimataifa.