Hamas yakataa mapatano ya aina yoyote na utawala wa Kizayuni
Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amepinga kufikiwa mapatatano yoyote kati ya harakati hiyo na utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kutoa suhula mbalimbali huko Ghaza mkabala na Hamas kusitisha uvurumishaji wa makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Suhail al HIndi ameeleza kuwa habari zilizotangazwa na duru za habari za Israel kwamba itatoa huduma za vifaa mbalimbali huko Ghaza iwapo Hamas itaacha kuvurumisha makombora kuelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hazina msingi wowote.
Mwakilishi wa Hamas amekanusha taarifa hizo za utawala wa Kizayuni baada ya kuvurumishwa Jumatano iliyopita kombora kuelekea katika kitongoji cha Asqalan kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakati Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni akihutubia.
Netanyahu ambaye alielekea katika kitongoji hicho kwa ajili ya kutoa hotuba na kampeni za uchaguzi alilazimika kuondoka huko na kupelekekwa kusikojulikana baada ya kuvurumishwa kombora.
Kuvurumishwa kombora hilo kumewatia kiwewe na woga Wazayuni wakihofia maisha yao na kuwapelekea viongozi wengi wa utawala huo kwa mara nyingine kuyatishia makundi ya muqawama kwamba wataanzisha siasa za kuwaua kigaidi viongozi wa Hamas ikiwa ni katika kujibu uvurumishaji huo wa kombora.