Shambulizi la maroketi lajiri karibu na ubalozi wa Marekani nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58649-shambulizi_la_maroketi_lajiri_karibu_na_ubalozi_wa_marekani_nchini_iraq
Eneo lenye ulinzi mkali la Green Zone karibu na ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad limeshambuliwa kwa maroketi usiku wa kuamkia leo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 21, 2020 07:35 UTC
  • Shambulizi la maroketi lajiri karibu na ubalozi wa Marekani nchini Iraq

Eneo lenye ulinzi mkali la Green Zone karibu na ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad limeshambuliwa kwa maroketi usiku wa kuamkia leo.

Ving'ora vya ambulensi vilisikika kwa masaa kadhaa usiku wa jana Jumatatu katika eneo hilo baada ya kujiri shambulio la maroketi, ingawaje idadi ya waliopoteza maisha au kujeruhiwa kwenye hujuma hiyo haijajulikana kufikia sasa.

Duru za habari zinaarifu kuwa, maroketi matatu aina ya Katyusha yamelenga eneo hilo, ambalo lina ofisi nyingi za kiserikali na kibalozi. Ofisi za balozi nyingi za nchi za Magharibi, Bunge na ofisi za Rais na Waziri Mkuu wa Iraq zinapatikana katika eneo hilo lenye ulinzi mkali.

Shambulizi hilo la maroketi limejiri wakati huu ambapo maandamano ya wananchi wa Iraq yameibuka tena katika maeneo mbalimbali nchini huo, ukiwemo mji mkuu Baghdad.

Eneo la Green Zone karibu na ubalozi wa US mjini Baghdad

Katika siku za hivi karibuni mikoa kadhaa ya Iraq ukiwemo wa Baghdad, imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali mbaya ya maisha, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali. 

Vyanzo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa, maandaano hayo ya Iraq hayakuibuliwa na wananchi wenyewe bali yalichochewa na maadui.