Jeshi la Israel latumia wanyama hai kufanyia majaribio silaha zake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61756-jeshi_la_israel_latumia_wanyama_hai_kufanyia_majaribio_silaha_zake
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel linawatumia wanyama walio hai kufanyia majaribio silaha zake kwa siri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 22, 2020 07:44 UTC
  • Jeshi la Israel latumia wanyama hai kufanyia majaribio silaha zake

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel linawatumia wanyama walio hai kufanyia majaribio silaha zake kwa siri.

Hayo yamefichuliwa na magazeti ya utawala huo haramu likiwemo la Yedioth Aharonoth.

Magazeti hayo yamenukuu ripoti ya shirika la kutetea haki za wanyama la “Let the Animals Live” ambayo imefuchua kuwa, Wizara ya Vita ya utawala huo imefanya majaribio zaidi ya elfu moja kwa kutumia hayawani tofauti ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Ripoti ya shirika hilo imebainisha kuwa, jeshi hilo la Kizayuni limetumia zaidi nguruwe katika majaribio ya silaha zake, kwa kuwa mnyama huyo ana mfumo wa kupumua unaofanana na wa binadamu.

Askari wa Israel wasivyowahurumia hata watoto wadogo

Nyaraka za shirika la kutetea haki za wanyama la “Let the Animals Live” zinasema utawalawa katili wa Israel umetumia baadhi ya majaribio hayo kutathmini radiamali ya binadamu kwa athari za milipuko na hivyo kuhatarisha uhai wa wanyama hao.

Utawala pandikizi wa Israel unawafanyia wananchi madhulumu wa Palestina kila aina ya ukatili, ukandamizaji na dhulma, mbele ya kimya cha taasisi za kutetea haki za binadamu na jamii ya kimataifa kwa ujumla.