Shambulizi la anga la Israel laua shahidi Wapalestina 4 Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63016-shambulizi_la_anga_la_israel_laua_shahidi_wapalestina_4_gaza
Wapalestina wanne wameuawa shahidi baada ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia kwa mabomu maeneo kadhaa ya Palestina huko mashariki mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Aug 25, 2020 03:28 UTC
  • Shambulizi la anga la Israel laua shahidi Wapalestina 4 Gaza

Wapalestina wanne wameuawa shahidi baada ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia kwa mabomu maeneo kadhaa ya Palestina huko mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Raia hao wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu waliouawa katika hujuma hiyo ya anga ya jeshi katili la Israel jana Jumatatu wametambuliwa kama Iyad Jamal al-Jidi, Muataz Amir al-Mubid, Yahya Fareed al-Mubid na Yaaqoub Zaydieh.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema "wanne hao wameuawa katika mripuko uliotokea wakiwa katika jitihada za kuwaondoa watenda jinai katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu."

Habari zaidi zinasema kuwa, Wapalestina hao wameuawa shahidi wakiwa katika kambi ya kijeshi ya harakati ya Jihadul Islami, katika mji wa Shejaiya, mashariki mwa Gaza.

Vijana wa Kipalestina waliouawa shahidi jana Jumatatu

Hata hivyo utawala haramu wa Israel unadai kuwa haujahusika na shambulizi hilo la anga, na eti vijana hao wa Kipalestina wameaga dunia baada ya kuripukiwa na bomu walilokuwa wakiliunda.

Eneo la Ukanda wa Gaza mbali na kushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya jeshi katili la Israel, kwa zaidi ya miaka 14 sasa limekuwa chini ya mzingiro wa anga, baharini na nchi kavu unaotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel.