Mwakilishi wa Hamas Tehran: Mapambano ndiyo njia pekee ya kushinda ubeberu
(last modified Tue, 15 Sep 2020 10:25:32 GMT )
Sep 15, 2020 10:25 UTC
  • Mwakilishi wa Hamas Tehran: Mapambano ndiyo njia pekee ya kushinda ubeberu

Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mjini Tehran amesema kuwa, mapambano na mshikamano wa Umma wa Kiislamu ndiyo njia pekee ya mataifa ya kuweza kuishinda Marekani na ubeberu wa kimataifa.

 Khaled al- Qaddumi amesema katika Kongamano la Kambi ya Kimataifa ya Vijana wa Muqawama lililofanyika jana katika mji wa Qum ulioko yapata kilomita 160 kusini mwa Tehran kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unawalenga wananchi katika nchi zilizochukua uamuzi wa kuanzisha uhusiano na utawala huuo.

Al Qaddumi amesema kuwa, nchi zilizoanzisha uhusiano na utawakla ghasibu wa Israel ni wasaliti wa Umma wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, kitendo hicho cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuanzisha uhusiano na utawala katili wa Israel hakitabakia kwa muda mrefu na kusisitiza kuwa, kuanzishwa uhusiano baina ya nchi za Imarati na Bahrain na utawala huo haramu hakutakuwa na matokeo mengine ghairi ya hasara za kimaada kwa viongozi wa nchi hizo. 

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem ambaye pia amehutubia Kongamano la Kambi ya Kimataifa ya Vijana wa Muqawama kwa njia ya video amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa: Hakuna nchi inayoweza kuwachukulia maamuzi Wapalestina badala ya Wapalestina wenyewe.  

Sheikh Naim Qassem

Sheikh Naim Qassem ameongeza kuwa, hatua ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na Israel ni usatiliti dhidi ya Palestina na Quds tukufu na haitakuwa na faida yoyote kwa Wapalestina.

Kongamana la Kambi ya Kimataifa ya Vijana wa Muqawama lilifanyika jana katika mji mtakatifu wa Qum likihudhuriwa na wanafikra mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu na makada wa kambi ya muqawama na mapambano dhidi ya ubeberu. 

Tags