Mbunge wa Iraq: Muswada wa kutimuliwa wanajeshi wa Marekani, utekelezwe haraka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64634-mbunge_wa_iraq_muswada_wa_kutimuliwa_wanajeshi_wa_marekani_utekelezwe_haraka
Mjumbe mmoja wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq amesisitiza kwamba, hakutakuwa na tofauti yoyote kubadilishwa sura ya rais wa Marekani, lililo muhimu kwa Iraq ni kutekelezwa muswada uliopasishwa na bunge la nchi hiyo wa kutimuliwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Nov 15, 2020 08:07 UTC
  • Mbunge wa Iraq: Muswada wa kutimuliwa wanajeshi wa Marekani, utekelezwe haraka

Mjumbe mmoja wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq amesisitiza kwamba, hakutakuwa na tofauti yoyote kubadilishwa sura ya rais wa Marekani, lililo muhimu kwa Iraq ni kutekelezwa muswada uliopasishwa na bunge la nchi hiyo wa kutimuliwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Kadhim al Rukabi, mjumbe wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq amesema kuwa, iwe Donald Trump au Joe Biden, yeyote atakayekuwa rais wa Marekani hatobadilisha kitu, na muswada wa kutimuliwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq lazima utekelezwe haraka wala hauwezi kufutwa. Amesema, suala la kutimuliwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ndiyo matakwa ya wananchi wa Iraq na kuongeza kuwa, serikali ya Baghdad inapaswa kuweka ratiba maalumu ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo. Wanajeshi vamizi wa Marekani wako katika maeneo mbalimbali ya Iraq kwa miaka mingi sasa. Mara chungu nzima wananchi wa Iraq wamekuwa wakipinga kuendelea kuwepo wanajeshi vamizi wa Marekani nchini mwao. Bunge la nchi hiyo limepasisha muswada wa kutimuliwa wanajeshi hao magaidi na kilichobakia hivi sasa ni utekelezaji tu.

Mashahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis

 

Uamuzi wa kuwatimua wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq ulichukuliwa baada ya wanajeshi hao vamizi kuwaua kigaidi, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH pamoja  Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolewa cha Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la Hashd al Shaabi, na wanamapambano wenzao wanane. Wanajeshi magaidi wa Marekani waliwaua kidhulma wanamapambano hao wa Kiislamu kwa kuwavizia wakiwa uraiani. Kilichowakasirisha zaidi wananchi wa Iraq ni kwamba Luteni Jenerali Qassem Soleimani, alikuwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq, lakini Trump na genge lake la magaidi hawakuheshimu haki ya kujitawala na kujiamulia mambo yake taifa la Iraq.