Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi: Askari wa Marekani lazima waondoke Iraq
Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq amesisitiza ulazima wa kutekelezwa mpango uliopitishwa na bunge wa kutaka askari wa jeshi la Marekani waondoke nchini humo.
Falih al-Fayyaz ametoa sisitizo hilo Jumapili alipohutubia mkoani Al Anbar kusini mwa Iraq na akaeleza kwamba, Wairaqi wamethibitisha kuwa, wao ni waaminifu kwa makamanda wao wanamapambano, hawakubali kuburuzwa na kulazmishwa, na nchi yao haitafuata na kutii utawala wa nchi nyingine.
Al Fayyaz aidha amelaani hatua ya wizara ya fedha ya serikali inayotawaliwa na migogoro ya rais Donald Trump wa Marekani ya kumwekea yeye vikwazo pamoja na mkuu wa vikosi vyote vya Al-Hashdu-Sha'abi Abu Fadak al Muhammadawi na akabainisha kwamba, Marekani haiko kwenye nafasi ya kuipa uwezo wa kutoa maagizo na amri kuhusiana na makamanada wa taifa la Iraq.
Askari wajeshi vamizi la Marekani wamepiga kambi nchini Iraq tangu mwaka 2003; na kambi yao kubwa kabisa ya kijeshi ya Ainul-Asad iko kwenye mkoa wa Al Anbar magharibi mwa nchi hiyo.
Wananchi wengi na makundi mbalimbali ya Wairaqi wanataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekanin waondoke nchini mwao; na bunge la Iraq pia limepitisha mpango kuhusiana na kuondoka askari hao magaidi katika ardhi ya nchi hiyo.../