Arab League yakiri kwamba kadhia ya Palestina imedharauliwa kwa makusudi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66150-arab_league_yakiri_kwamba_kadhia_ya_palestina_imedharauliwa_kwa_makusudi
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amelaumu vikali misimamo ya baadhi ya nchi kuhusu kadhia ya Palestina na kulalamika kuwa, taifa la Palestina limedharauliwa kwa makusudi.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 27, 2021 03:56 UTC
  • Arab League yakiri kwamba kadhia ya Palestina imedharauliwa kwa makusudi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amelaumu vikali misimamo ya baadhi ya nchi kuhusu kadhia ya Palestina na kulalamika kuwa, taifa la Palestina limedharauliwa kwa makusudi.

Televisheni ya Rusia al Yaum imeripoti habari hiyo leo na kumnukuu Ahmad Abul Gheit akisema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika kwa njia ya Intaneti na kuongeza kuwa, katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Donald Trump huko Marekani, wananchi wa Palestina wamekumbwa na mashinikizo makubwa yasiyokadirika. Ameitaka serikali mpya ya Marekani kurekebisha hali hiyo na kutoendeleza siasa hizo za Donald Trump.

Amesema, tunaitaka serikali mpya ya Marekani iachane na siasa zisizokubalika zilizofuatwa na nchi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita kuhusu Palestina. Bali ifuate siasa ambazo zitawapa matumiani wananchi wa Palestina na kuwafanya waelewe kuwa jamii ya kimatafa iko pamoja nao katika mapambano yao ya miaka mingi ya kupigania ukombozi na uhuru wao.

Ahmad Abul Gheit, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu 

 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amelalamikia pia kuweko misimamo isiyo ya kiuadilifu kuhusiana na kadhia ya Palesitna na kudharauliwa kwa makusudi suala hilo huku utawala wa Kizayuni ukiendelea kuwatwisha masuala yasiyobebeka wananchi wa Palestina.

Mwishoni mwa hotuba yake, Abul Gheit ameitaka jamii ya kimataifa isimame imara kukabiliana na uamuzi wa Marekani wa kutambua Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni akisisitiza kuwa, eneo hilo takatifu ndio mji mkuu usiopingika wa Palestina, si wa utawala wa Kizayuni.