Wapalestina 160 wanateseka katika jela za Saudi Arabia hivi sasa
(last modified Sun, 20 Jun 2021 02:23:17 GMT )
Jun 20, 2021 02:23 UTC
  • Wapalestina 160 wanateseka katika jela za Saudi Arabia hivi sasa

Shirika la habari la "Palestine Today" limetangaza kuwa, sasa hivi kuna Wapalestina 160 wanaoteseka katika jela za ukoo wa Aal Saud nchini Saudi Arabia. Wapalestina hao wanashikiliwa kwenye jela hizo za Saudi Arabia kwa tuhuma za kuwa wanachama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Shirika hilo lilitangaza habari hiyo jana na kunukuu kundi la haki za binadamu la "Muutaqal al Ra'ay" likiandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, uchunguzi uliofanyika unaonesha kuwa, sasa hivi kuna wafungwa 160 wa Kipalestina katika jela moja ya eneo la Abha la kusini magharibi mwa Saudi Arabia.

Kundi hilo limefichua pia kuwa, mmoja wa Wapalesitna wanaoshikiliwa kwenye jela hiyo ya ukoo wa Aal Saud huko Saudia ni Dk ‪Mohammad Khezri‬, mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina nchini Saudi Arabia ambaye hivi sasa hali yake ni mbaya kutokana na ugonjwa.

Jinai zinazofanywa dhidi ya Saudi Arabia dhidi ya Waislamu ni kubwa sana

 

Harakati ya HAMAS na taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa likiwemo shirika la Amnesty International yamekuwa yakisisitiza mara kwa mara juu wa wajibu wa kuachiliwa huru Wapalestina wanashikiliwa kidhulma huko Saudi Arabia, lakini ukoo wa Aal Saud unaendelea kufanya ukaidi na hauwaachilii huru Wapalestina hao.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unadai kuwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na makundi mengine ya muqawama yanayopigania ukombozi wa Palestina kuwa eti ni makundi ya kigaidi. 

Cha kusikitisha ni kuwa nchi kama Saudi Arabia zinatekeleza kivitendo mtazamo huo wa utawala wa Kizayuni wa kuwakamata na kuwatesa wanamapambano wa Palestina kwa sababu ya kusimama kwao kidete kupambana na dola pandikizi la Israel.

Tags