Sergei Lavrov: Kuondoka Marekani nchini Afghanistan ni kukiri kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72116-sergei_lavrov_kuondoka_marekani_nchini_afghanistan_ni_kukiri_kushindwa
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kimsingi ni kukiri wazi kugonga mwamba majukumu yake katika nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 08, 2021 08:16 UTC
  • Sergei Lavrov: Kuondoka Marekani nchini Afghanistan ni kukiri kushindwa

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kimsingi ni kukiri wazi kugonga mwamba majukumu yake katika nchi hiyo.

Sergei Lavrov ameeleza kwamba, Marekani si tu kwamba, inaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan, bali kwa hatua yake hiyo imekiri kwamba, imeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika nchi hiyo.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesisitiza kwamba, hatua hiyo ni sawa na Washington kukubali kuwa imeshindwa mtawalia kwa muda wa miaka 20 ya kuwepo kwake kijeshi nchini Afghanistan.

Marekani baada ya kukiuka mara kadhaa ahadi yake ya kuwaondoa wanajeshi wake huko nchini Afghanistan, sasa imetangaza kuwa, hadi kufikia Septemba 11 mwaka huu itakuwa imewaondoa wanajeshi hao kutoka nchini humo.

Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia 

 

Marekani inaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan katika hali ambayo, kuwepo kwao kwa miaka 20 katika nchi hiyo hakujawa na natija yoyote ghairi ya mauaji ya makumi ya maelfu ya wananchi wa Afghanistan, kuhairibiwa miundomsingi ya nchi na kuongezeka viitendo vya ugaidi.

Mnamo mwaka 2001, Marekani na waitifaki wake waliishambulia na kuivamia kijeshi Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha amani nchini humo; hata hivyo uvamizi huo uliitumbukiza Afghanistan kwenye lindi la vita na mapigano, kuangamiza miundomsingi yake ya kiuchumi  na kushamirisha machafuko, ugaidi na uzalishaji wa madawa ya kulevya katika nchi hiyo