Nabih Berri apendekeza mpango wa kuinasua Lebanon kwenye mkwamo wa kisiasa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7390-nabih_berri_apendekeza_mpango_wa_kuinasua_lebanon_kwenye_mkwamo_wa_kisiasa
Spika wa Bunge la Lebanon amependekeza mpango wa vipengee vitatu kwa lengo la kuinasua nchi hiyo kwenye mkwamo wa kisiasa wa kubaki bila ya kuwa na Rais kwa takribani miaka miwili sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 19, 2016 23:36 UTC
  • Nabih Berri apendekeza mpango wa kuinasua Lebanon kwenye mkwamo wa kisiasa

Spika wa Bunge la Lebanon amependekeza mpango wa vipengee vitatu kwa lengo la kuinasua nchi hiyo kwenye mkwamo wa kisiasa wa kubaki bila ya kuwa na Rais kwa takribani miaka miwili sasa.

Nabih Berri ametangaza mpango huo ambao unajumuisha pendekezo la kufikiwa makubaliano juu ya sheria mpya ya kumchagua rais, kufanyika uchaguzi wa bunge kulingana na sheria iliyopo na kushiriki upya katika mazungumzo ya Doha, Qatar.

Mpango wa awamu tatu wa mazungumzo ya Doha unajumuisha muundo wa serikali ya Muungano na kurekebishwa sheria ya uchaguzi wa bunge na kuchaguliwa rais wa Lebanon.

Tangu tarehe 25 Mei 2014 baada ya kumalizika kipindi cha urais wa Michel Suleiman, Lebanon imekumbwa na ombwe la kisiasa kwa kubaki bila ya kuwa na rais kutokana na bunge kushindwa hadi sasa kufikia mwafaka juu ya mtu atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Michel Suleiman.

Hadi sasa kuna wanasiasa wawili tu waliosalia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo ambao ni Suleiman Frangieh na Michel Aoun.../