Hizbullah: Vikwazo vya Marekani haviathiri mapambano ya Walebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81048-hizbullah_vikwazo_vya_marekani_haviathiri_mapambano_ya_walebanon
Mbunge wa harakati ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon amesema vikwazo vya Marekani havina taathira yoyote katika mapambano ya Kiislamu au muqawama na kuongeza kuwa, Hizbullah ina njia mbalimbali za kusimama kidete na kukabiliana na mashinikizo ya maadui.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2022 10:46 UTC
  • Hizbullah: Vikwazo vya Marekani haviathiri mapambano ya Walebanon

Mbunge wa harakati ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon amesema vikwazo vya Marekani havina taathira yoyote katika mapambano ya Kiislamu au muqawama na kuongeza kuwa, Hizbullah ina njia mbalimbali za kusimama kidete na kukabiliana na mashinikizo ya maadui.

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Lebanon ikiwa ni katika sera zake za kuidhoofisha nchi hiyo hasa katika sekta ya kuchimba mafua na gesi.

Hassan Fadhlullah mwanachama wa mrengo wa 'Watiifu kwa Muqawama' katika Bunge la Lebanon ametoa wito kwa Walebanoni kutoiamini Marekani hata kidogo. Aidha amefichua kuwa Marekani inalenga kujipenyeza katika mfumo wa benki nchini Lebanon ili kuhakikisha kuwa inadhibiti kila kitu kinachofanyika katika benki za nchi hiyo.

Maandamano Lebanon

Mbunge hiyo wa Hizbullah amesema Wizara ya Fedha ya Marekani inaiwekea vikwazo Lebanon na watu wake ili kushinikiza harakati za mapambano ya Kiislamu lakini wafahamu kuwa mashinikizo hayo hayaathiri muqawama hata kidogo. Amesema kinyume cha wanavyotarjia Wamarekani, vikwazo hivyo vitawafanya Walebanoni wafungamana zaidi na harakati ya mapambano na hivyo Marekani haitapata chochote isipokuwa kupoteza matumaini na kusambaratika vikwazo vyake.

Hivi karibuni kumeshuhudiwa maandamano Lebanon kutokana na na mgogoro katika mfumo wa kifedha na uchumi. Walebanoni wanalalamikia ufisadi katika taasisi za serikali huku wakikabiliwa na vikwazo vya Marekani.