White House yakosolewa kwa mwenendo wake mbaya dhidi ya Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i820-white_house_yakosolewa_kwa_mwenendo_wake_mbaya_dhidi_ya_waislamu
Wakosoaji na makundi mbalimbali ya Kiislamu nchini Marekani yamekosoa mwenendo wa Ikulu ya Rais wa Marekani White House na viongozi wa nchi hiyo wakisema unazidisha chuki na uhasama dhidi ya Waislamu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 08, 2016 06:58 UTC
  • White House yakosolewa kwa mwenendo wake mbaya dhidi ya Waislamu

Wakosoaji na makundi mbalimbali ya Kiislamu nchini Marekani yamekosoa mwenendo wa Ikulu ya Rais wa Marekani White House na viongozi wa nchi hiyo wakisema unazidisha chuki na uhasama dhidi ya Waislamu nchini humo.

Mkuu wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) Daud Waliid amesema Rais Barack Obama daima amekuwa wakiwachukuza Waislamu na kuathiri vibaya jamii ya nchi hiyo kutokana na maamuzi yake ya kisiasa.

Mkuu wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu amesema kuwa, katika kipindi cha uongozi wa Rais Barack Obama kiwango cha hujuma dhidi ya Uislamu kimeongeza sana nchini Marekani.

Wiki iliyopita kiongozi huyo alifanya jaribio la kusafisha sura ya serikali yake mbele ya Waislamu kwa kutembelea Msikiti wa Baltimore kwenye jimbo la Maryland. Wakati huo baadhi ya mitandao ya kijamii iliandika kuwa, mwaka 2014 Rais Barack Obama aliipatia Israel zana na silaha zote ilizohitajia kwa ajili ya kuwakandamiza Waislamu wa Palestina.

Akiwa msikitini hapo Obama alikabiliwa na mabango yaliyokuwa na maandishi: "Obama umechelewa sana", "jela ya Guantanamo bado haijafungwa" "ndege zisizo na rubani za Marekani zingali zinaleta ujumbe wa mauati" na Marekani inaunga mkono vita katika eneo lote la Mashariki ya Kati na Afrika".