Makundi ya Palestina yapongeza kufanyika kwa amani uchaguzi wa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83782-makundi_ya_palestina_yapongeza_kufanyika_kwa_amani_uchaguzi_wa_lebanon
Wakuu wa makundi mbalimbali ya Palestina wametoa tamko la pamoja na kulipongeza taifa la Lebanon kwa kufanya uchaguzi kwa amani na wameliombea taifa hilo ustawi na maendeleo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 19, 2022 02:41 UTC
  • Makundi ya Palestina yapongeza kufanyika kwa amani uchaguzi wa Lebanon

Wakuu wa makundi mbalimbali ya Palestina wametoa tamko la pamoja na kulipongeza taifa la Lebanon kwa kufanya uchaguzi kwa amani na wameliombea taifa hilo ustawi na maendeleo.

Shirika rasmi la habari la Lebanon limeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa ya pamoja ya makundi hayo ya Palestina iliyotolewa jana Jumatano ikisema kuwa, taifa la Palestina linataraji Lebanon itatoka kwenye mgogoro wa kisaisa, kiuchumi na kijamii, umoja wa kweli wa kitaifa utapatikana na watu wote wataishi kwa salama na amani nchini humo.

Uchaguzi wa lebanon umefanyika baada ya miezi kadhaa ya mkwamo. Uchaguzi huo wa bunge ulinza siku ya Jumapili katika maeneo taofauti ya Lebanon na umemalizika kwa utulivu na amani.

Lebanon muda wote iko mstari wa mbele katika kuunga mkono ukombozi wa Palestina

 

Katika tamko lao hilo, wakuu wa makundi ya Palestina wamesema pia kuwa, wanatumai uchaguzi huo utakuwa na matunda mazuri kwa hali ya wakimbizi wa palestina waishio Lebanon, kwani daima nchi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuinda na kuunga mkono kadhia ya Palestina, haki za taifa la Palestina na umoja na mshikamano katika ulimwengu wa kiarabu. 

Jumanne, matokeo yote ya ucahguzi huo yalitangazwa pamoja na majina ya wagombea wote walioshinda kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi wa hivi sasa wa Bunge la Lebanon ni matunda ya muswada wa marekebisho yaliyotakiwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kwa ajili ya kuisaidia Lebanon. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa Lebanon iko kwenye mgogoro wa kiuchumi.