Walebanon wataka kutimuliwa balozi wa Saudi Arabia mjini Beirut
(last modified Wed, 02 Nov 2022 13:39:51 GMT )
Nov 02, 2022 13:39 UTC
  • Walebanon wataka kutimuliwa balozi wa Saudi Arabia mjini Beirut

Wananchi wa Lebanon wametoa mwito wa kutimuliwa nchini humo balozi wa Saudi Arabia wakimtuhumu kwamba, amekuwa akiingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Hasira za wananchi wa Lebanon zililipuka pale Walid al-Bukhari, balozi wa Saudi Arabia mjini Beirut aliposhiriki katika hafla ya kikabila.

Washiriki wa hafla hiyo walikasirika na kuanza kutoa nara baada ya balozi huyo wa Saudia kuwasili katika hafla hiyo.

Wananchi hao wameitaka serikali ya Lebanon kumtimua balozi huyo wa Saudia.

Balozi huyo ambaye alipanga kukutana katika hafla hiyo na viongozi tofauti wa kikaumu alilazimika kufuta ratiba hiyo kwa sababu za kiusalama.

Bendera za Saudi Arabia na Lebanon

 

Kabla ya hapo, balozi huyo wa Saudia mjini Beirut amewahi kushiriki katika hafla mbalimbali kama hizo na kujaribu kuwashawishi viongozi wa kikaumu nchini humo ili wawe na mtazamo chanya na utawala wa Aal Saud.

Wiki iliyopita baada ya kushaididi ukosoaji dhidi ya harakati zake binafsi na siaza za Saudi Arabia huko Beirut, aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwamba, Riyadh haitaki kuingilia masuala ya ndani ya Lebanon. Wananchi wa Lebanon na hata wanasiasa wa nchi hiyo wamekuwa wakiituhumu Saudi Arabia kwamba, inaingilia masala ya ndani ya nchi yao na kwamba, Riyadh pamoja na washirika wake kama Marekani ndio wahusika wa mgogoro wa sasa wa kiuchumi na kisiasa.

Tags