Qatar imewanasa majasusi kadhaa wa Israel raia wa India
(last modified Fri, 11 Nov 2022 03:09:06 GMT )
Nov 11, 2022 03:09 UTC
  • Qatar imewanasa majasusi kadhaa wa Israel raia wa India

Shirika la Intelijensia la Qatar limewakamata maafisa wanane wa zamani wa Jeshi la Wanamaji wa India nchini Qatar wanaoshukiwa kufanya ujasusi kwa manufaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa tovuti huru ya habari Al-Watan, maafisa hao wanane wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la India waliajiriwa na kampuni binafsi nchini Qatar iitwayo Dahra Global Technology and Consulting Services, ambayo hutoa mafunzo na huduma zikiwemo za usaidizi na matengenezo ya vifaa kwa Jeshi la Wanamaji la Qatar. 
Tovuti ya Al-Watan imeripoti kuwa, mashtaka yanayohusishwa dhidi ya maafisa hao wa zamani wa jeshi la wanamaji la India bado hayajajulikana, lakini taarifa zilizofichuliwa zinaonyesha kuwa watu hao wamekuwa wakifanya ujasusi kwa manufaa ya utawala haramu wa Israel.
Historia ya uhusiano wa ujasusi baina ya India na Israel

Kulingana na ripoti hiyo, mnamo mwishoni mwa mwezi Septemba, serikali ya Doha iliwaruhusu maafisa hao wa zamani wa jeshi la wanamaji la India waliokamatwa kupiga simu kwa familia zao.

Imeelezwa kwamba, watu hao wamekuwa wakifanya kazi katika kampuni hiyo binafsi ya Qatar ya Dahra Global Technology and Consulting Services kwa takriban miaka minne hadi sita sasa.
Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Oktoba, India ilituma afisa wake mmoja mwandamizi huko Doha ili kusaidia maafisa wa ubalozi wake kufanikisha kuachiliwa huru raia wake hao wanaoshikiliwa kwa ujasusi.../