-
Umoja wa Mataifa: Kuwanyima Wapalestina kupata chakula ni uhalifu wa kivita
Jun 04, 2025 09:33Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, akikosoa jinsi misaada inavyosambazwa katika Ukanda wa Gaza, ametangaza kuwa, kuwanyima raia kupata chakula huko Gaza kunaweza kuwa uhalifu wa kivita.
-
Kwa nini mashinikizo dhidi ya Netanyahu hayafanyi kazi?
Jun 04, 2025 07:32Mauaji ya Wapalestina wanaoishi Gaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni yangali yanaendelea, huku nchi na jumuiya mbalimbali za kimataifa zikitoa wito wa kukomeshwa mauaji hayo mara moja.
-
Jordan yawashutumu walowezi wa Israel kuingia kwa nguvu Al-Aqsa
Jun 03, 2025 23:17Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni ya Jordan imelaani vikali vitendo vya mara kwa mara vya walowezi wa Kizayuni kuvamia Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Israel imeua Wapalestina zaidi ya 54,500 huko Gaza tangu Oktoba 2023
Jun 03, 2025 23:03Idadi ya vifo vya Wapalestina katika vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea Gaza, ambavyo vilianza Oktoba 7 2023, sasa imepindukia 54,500. Aghalabu ya waliouawa ni wanawake na watoto. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya Ukanda huo iliyotolewa Jumanne.
-
WFP: Watu milioni mbili wanataabika na njaa Gaza
Jun 03, 2025 07:40Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa zaidi ya watu milioni mbili katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na njaa kali, huku wengi wao wakikaribia kukumbwa na ukame na ukata wa ajabu.
-
Jeshi la Israel lapata kipigo kingine kikubwa kutoka kwa HAMAS
Jun 03, 2025 03:34Wanajeshi vamizi wa Israel wameingia kwenye mtego uliotegwa na Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS huko Jabalia, kaskazini mwa Ghaza na wamepoteza wanajeshi kadhaa.
-
Yemen: Tumeupiga tena Uwanja wa Ndege wa Israel kwa kombora la Zulfiqar
Jun 03, 2025 03:34Msemaji wa jeshi la Yemen, Meja Jenerali Yahya Saree ametangaza kuwa, usiku wa kuamkia leo Jumanne, jeshi hilo limeupiga tena Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa Israel huko Tel Aviv kwa kutumia kombora la balestiki la Zulfiqar.
-
Yemen yataka makampuni ya kigeni yaondoke 'Israel', mashambulizi yatashadidi
Jun 02, 2025 07:52Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, Mahdi al-Mashat, ametoa onyo kali kwa makampuni ya kigeni yanayowekeza katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepewa jina bandia la Israel, akibainisha kuwa hatua mpya za kijeshi za Yemen ziko mbioni kuchukuliwa ikiwa uvamizi wa Gaza utaendelea.
-
Hamas: Jinai za Israel Gaza zinashinda uhalifu wa Wanazi
Jun 02, 2025 03:14Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amelaani shambulizi la karibuni la Israel dhidi ya wananchi wa Kipalestina wenye njaa waliouawa shahidi wakiendea chakula cha msaada kusini mwa Gaza, akibainisha kwamba mauaji haya yanatuma ujumbe wa wazi kwa ulimwengu wa Kiislamu kwamba wakati umefika wa kusimama dhidi ya wauaji.
-
Uwanja wa Ben Gurion wapigwa tena kombora la hypersonic
Jun 02, 2025 03:13Jeshi la Yemen limesema kuwa limeanzisha tena operesheni mpya za kulipiza kisasi dhidi ya maeneo yanayolengwa na Israel ndani kabisa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ili kukabiliana na jinai na uchokozi unaoendelea dhidi ya Wapalestina wa Gaza.