-
Ansarullah Yemen: Hakuna meli ya Saudi Arabia inayoruhusiwa kupita Lango Bahari la Bab al-Mandab
Jul 27, 2026 10:14Harakati ya Ansarullah yaYemen imesema kuwa Mlango Bahari wa Bab al-Mandab umefungwa kikamilifu kwa Saudi Arabia, huku ikisisitiza msimamo wake kuhusu hatua zinazohusiana na usalama wa njia hiyo muhimu ya baharini.
-
Hamas yalaani hatua za 'Zio-American' zinazolenga UNRWA, yahimiza hatua za kimataifa
Jul 27, 2026 03:52Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani hatua mpya za Marekani na Israel zinazolenga Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), likitaka kuchukuliwe hatua za dharura za kimataifa dhidi ya kampeni ya "Wazayuni-Marekani" ya kutaka kulisambaratisha shirika hilo.
-
Walowezi wa Israel wachoma misikiti ya Ukingo wa Magharibi
Jul 27, 2026 03:48Walowezi wa Kiisraeli wamevamia misikiti miwili, mmoja uliokuwa ukijengwa, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuichoma moto katika kile kinacholaaniwa kama kampeni ya kimfumo inayolenga haki za kidini za Wapalestina.
-
Wizara ya Afya Gaza: Israel imeuwa Wapalestina wengine 9 Gaza; Vifo vyapindukia 73,300
Jul 26, 2026 13:14Wapalestina wengine tisa wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza katika saa 24 zilizopita.
-
Francesca Albanese atoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha utawala wa Kizayuni
Jul 26, 2026 02:48Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika Ardhi za Palestina Zinazokaliwa kwa Mabavu, Francesca Albanese, ameyataja mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa ni "mauaji ya kimfumo", na kuitaka jamii ya kimataifa kuweka mara moja vikwazo vya silaha pamoja na kusitisha biashara na utawala huo.
-
Zaidi ya wanamichezo 1,000 wa Kipalestina wameuawa shahidi na Israel
Jul 26, 2026 02:46Shirikisho la Soka la Palestina limetangaza kuwa wanamichezo 1,013 wa Kipalestina wameuawa shahidi tangu kuanza vita dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba 2023, kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.
-
Jeshi la Yemen latekeleza hujuma ya makomora dhidi ya Saudi Arabia
Jul 25, 2026 11:15Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimefyatua makombora na kupiga kituo kikuu cha kijeshi cha anga katika jimbo la Asir, kusini mwa Saudi Arabia, ikiwa ni hatua ya kujibu mapigo dhidi ya mashambulizi ya kijeshi ya hivi karibuni ya utawala wa Saudia pamoja na mzingiro unaoendelea dhidi ya nchi hiyo.
-
Afisa wa UN alaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina
Jul 25, 2026 11:08Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa, Francesca Albanese, amelaani vikali wimbi kubwa la ghasia zinazotekelezwa na walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika maeneo yote ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel.
-
Hamas: Kuongezeka mashambulizi dhidi ya Gaza ni jaribio la kuua makubaliano ya kusitisha mapigano
Jul 24, 2026 07:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kwamba mashambulizi makubwa ya anga ya utawala wa Israel eneo la Ukanda wa Gaza katika saa kadhaa zilizopita ni mwendelezo wa vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wasio na hatia na msisitizo wa kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Iran yashambulia ngome za Marekani nchini Kuwait na Jordan yasema ni haki kisheria, kidini na kimantiki
Jul 23, 2026 11:53Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limethibitisha kufanya mashambulio dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Kuwait na Jordan, likisisitiza kuwa kulenga kambi zinazotumiwa katika operesheni dhidi ya Iran ni “haki ya Iran ya kisheria, kidini, na kimantiki.”