-
Waziri mwenye itikadi kali wa Israel aamuru kubomolewa nyumba za Wapalestina mwezi wa Ramadhani
Mar 06, 2023 23:04Waziri mwenye misimamo ya kupindukia mipaka wa usalama wa ndani wa utawala wa haramu wa Israel ametoa amri ya kuharibiwa nyumba za wananchi wa Palestina katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Iraq: Katika siku za usoni tutakuja kukabiliwa na kizazi kipya cha DAESH (ISIS)
Mar 06, 2023 06:29Msemaji wa Kamandi Kuu ya vikosi vya ulinzi vya Iraq ametoa indhari kwa kusema: "katika miaka michache ijayo, tutakabiliana na kizazi kipya cha magaidi wa DAESH (ISIS), tukiwa hatuna taarifa zozote za kukitambua kizazi hicho".
-
Jumuiya ya al-Wifaq: Bahrain imegeuzwa na kufanywa kaburi la haki za binadamu
Mar 06, 2023 04:11Jumuiya ya Kitaifa na Kiislamu nchini Bahrain ya Al-Wifaq imetangaza kuwa, nchi ya Bahrain imegeuzwa na kufanywa kuwa kaburi la haki za binadamu na kwamba, haipaswi kughafilika na hatua zinazochukuliwa na utawala huo ambazo ni kinyume cha sheria.
-
Walowezi wa Kizayuni waendeleza vitendo vya kuuvamia msikiti wa al-Aqswa
Mar 06, 2023 04:04Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.
-
Saudia yapiga marufuku kutangaza Swala za mwezi wa Ramadhani katika vyombo vya habari
Mar 05, 2023 23:01Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia imepiga marufuku utangazaji wa ibada ya Swala za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo.
-
Mash'al: Kuanzisha uhusiano na Israel umeisababishia Palestina dhiki
Mar 05, 2023 07:28Kiongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nje ya nchi ameyakosoa baadhi ya madola ya Kiarabu kwa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kusisitiza kuwa, ushirikiano na utawala huo wa Kizayuni haujakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuwasababishia Wapalestina dhiki na matatizo.
-
US yaendelea kuiba mafuta ya Syria licha ya kukumbwa na zilzala
Mar 05, 2023 07:19Marekani kwa kushirikiana na mamluki wa Kikurdi imeendelea kuiba mafuta ya Syria, wakati huu ambapo nchi hiyo ya Kiarabu inajaribu kujinasua kutoka kwenye misukosuko na changamoto zinazotokana na matetemeko ya ardhi yaliyoua maelfu ya watu nchini humo.
-
Afisa wa Haki za Binadamu UN: Hali katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni janga
Mar 05, 2023 04:40Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu ametoa tahadhari kutokana na wito wa waziri wa utawala wa Israel ambaye ametaka kuangamizwa kijiji kizima cha Wapalestina.
-
Ziyad al-Nakhalah: Wapalestina hawataruhusu mipango ya Wazayuni Palestina itekelezwe kivitendo
Mar 05, 2023 00:28Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa, wapiganaji shupavu wa Paalestina katu hawataruhusu mipango michafu ya Wazayuni huko Palestina itekelezwe kivitendo.
-
Afisa wa Yemen: Madai ya Uingereza kukamata silaha za Iran ni upuuzi mtupu
Mar 04, 2023 07:51Naibu Waziri wa Habari wa Yemen, Fahmi al-Yousefi amepuuzilia mbali madai ya jeshi la wanamaji la Uingereza kuhusu eti kukamatwa boti iliyokuwa inasafirisha silaha za Iran katika pwani ya Ghuba ya Oman na kuyataja kuwa ya kipuuzi.