-
POLITICO: Saudia kutumia mabilioni ili iwe mwenyeji wa Kombe la Dunia
Feb 11, 2023 23:06Saudi Arabia imeripotiwa kutoa pendekezo kwa siri la kuwa tayari kugharamia ujenzi wa miundombinu yote kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotazamiwa kufanyika Ugiriki na Misri mwaka 2030.
-
Syria yakosoa 'upotoshaji' wa Marekani kuhusu kuondoa vikwazo
Feb 11, 2023 23:05Serikali ya Syria imekosoa vikali hatua ya Marekani ya kutangaza kuisimamishia vikwazo nchi hiyo ya Kiarabu kwa muda wa miezi sita, eti ili kuruhusu kupelekwa misaada ya dharura katika taifa hilo lililokumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi hivi karibuni.
-
Baada ya kupita siku 5, manusura wa tetemeko la ardhi waendelea kupatikana vifusini nchini Uturuki
Feb 11, 2023 08:27Watu kadhaa wameokolewa leo nchini Uturuki kwa kutolewa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, wakati vikosi vya uokoaji kutoka nchi mbalimbali duniani vikiongeza kasi ili kujaribu kuokoa maisha ya watu zaidi baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumatatu kusini mwa nchi hiyo na katika nchi jirani ya Syria.
-
Idadi ya waliofariki dunia yapindukia 24,000 zilzala ya Syria na Uturuki, matumaini ya kupata manusura zaidi yanafifia
Feb 11, 2023 03:56Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa na zizlala ya Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 5 baada ya maafa ya tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 24,000 na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine.
-
Mshauri wa Bashar Assad: Vikwazo vya Magharibi vinatatiza utoaji wa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi
Feb 11, 2023 03:53Mshauri wa vyombo vya habari wa Rais wa Syria amesema: Kinachozidisha hali mbaya ya sasa kwa watu waliokumbwa na janga la tetemeko la ardhi ni vikwazo vya Marekani na Ulaya dhidi ya Syria.
-
Askari katili wa Israel wamewaua watoto tisa wa Kipalestina mwaka huu
Feb 10, 2023 22:52Wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wamewapiga risasi na kuwaua Wapalestina 42 wakiwemo watoto tisa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
-
Hizbullah: Tupo tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Syria
Feb 10, 2023 03:27Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikisisitiza uungaji mkono wa pande zote wa muqawama wa Lebanon kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi huko Syria na kusisitiza kuwa itatumia suhula zake zote kuisaidia na kuihudumia serikali na wananchi wa Syria katika mazingira haya magumu baada ya zilzala.
-
Vikwazo na ugaidi; matatizo mawili yanayopelekea wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria kutofikishiwa misaada ya kibinadamu
Feb 10, 2023 03:13Serikali ya Syria iko mbioni kuwafikishia misaada ya kibidanamu waathirika na wahanga wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini humo hivi karibuni lakini pamoja na hayo inakabiliwa na vizuizi vikuu viwili ambavyo ni vikwazo na ugaidi na hivyo kufanya shughuli zake katika uwanja huo kuwa ngumu.
-
Duru mpya ya mazungumzo baina ya Iran na Saudia kufanyika hivi karibuni Baghdad, Iraq
Feb 09, 2023 22:56Waziri Mkuu wa Iraq ametangaza kuwa duru mpya ya mazungumzo kati ya Iran na Saudi Arabia itafanyika hivi karibuni mjini Baghdad.
-
Rais Assad: Marekani inazishinikiza nchi nyingi zisiwasaidie waathirika wa tetemeko la ardhi Syria
Feb 09, 2023 10:15Rais Bashar al-Assad wa Syria amefichua kuwa Marekani inatoa mashinikizo kwa nchi zinazotaka kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Syria. Assad ameyasema hayo katika mkutano na ujumbe wa mawaziri kadhaa wa Lebanon.