-
Israel yafanya mashambulio ya kinyama Ghaza, yaua Wapalestina 28 na kujeruhi 77
Nov 20, 2025 02:39Wapalestina wasiopunguua 28 wameuawa shahidi katika wimbi jipya la mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza, yakiwa ni moja ya ukiukaji mkubwa zaidi wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani na kuanza kutekelezwa mwezi uliopita wa Oktoba.
-
Wataalamu: Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Gaza ni la kuwakoloni Wapalestina
Nov 19, 2025 23:29Azimio jipya la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), linaloruhusu kile kinachoitwa kikosi cha kimataifa kutumia “mbinu zozote zinazohitajika kutekeleza wajibu wake” katika Ukanda wa Gaza limeelezwa na wataalamu kama sura nyingine ya “ukoloni” katika historia ya Palestina.
-
Kwa nini hati ya makubaliano ya kijeshi kati ya India na utawala wa Kizayuni ni hatua ya kuleta ukosefu wa utulivu Asia?
Nov 19, 2025 23:23India na utawala wa Kizayuni wa Israel zimepanua ushirikiano wao wa kijeshi na kiviwanda kwa kutiliana saini hati mpya ya maelewano na ushirikiano.
-
Kampuni ya silaha ya Israel ya Elbit imeingiza mapato makubwa wakati wa mauaji ya kimbari ya Gaza
Nov 19, 2025 09:00Kampuni ya Israel inayoongoza kwa utengenezaji wa silaha, Elbit Systems, imetangaza ongezeko kubwa la faida iliyopatikana katika muda wa robo mwaka kufuatia miezi kadhaa ya ushiriki wa kampuni hiyo katika mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza kupitia utoaji silaha, zana za kijeshi na mifumo ya ufuatiliaji, huku ikipata mikataba mipya barani Ulaya.
-
Watu 15 wauawa katika hujuma ya anga ya Israel katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina huko Lebanon
Nov 19, 2025 03:28Utawala wa Israel umefanya mashambulizi ya anga na kuuwa watu wasiopungua 15 kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Kipalestina kusini mwa Lebanon.
-
'Siku ya fedheha’: Afisa wa zamani wa haki za binadamu wa UN akosoa azimio la UNSC kuhusu Gaza
Nov 19, 2025 03:26Afisa wa ngazi ya juu wa zamani wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amelaani hatua ya Baraza la Usalama la umoja huo ya kupitishaa azimio linalounga mkono mpango wa Marekani wa kuanzisha kikosi cha kimataifa cha kurejesha utulivu katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, akiitaja kura hiyo kuwa ni "siku ya fedheha" kwa chombo hicho cha dunia.
-
Umoja wa Mataifa: Wayemen milioni 17 wanakabiliwa na njaa kali
Nov 18, 2025 07:19Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake ya hivi punde kwamba raia milioni 17 wa Yemen wanakabiliwa na njaa kali, na idadi hii inatarajiwa kuongezeka.
-
Ukata na umaskini wa Wazayuni umeongezeka kwa theluthi nzima baada ya Oktoba 7
Nov 17, 2025 22:53Mfumuko wa bei na gharama ya maisha zinazidi kupanda huko Israel. Huku hali ikiwa hivyo ripoti rasmi ya Taasisi ya Bima ya Israel inaoneesha kwamba umaskini umeongezeka kwa zaidi ya theluthi moja kwa wakazi wa utawala huo baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa ya Oktoba 7, 2023.
-
Kwa nini Hamas na makundi ya muqawama ya Palestina yanapinga azimio lililopendekezwa na Marekani?
Nov 17, 2025 07:22Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza katika taarifa yake kwamba makundi na harakati za Palestina zimewasilisha waraka kuhusu rasimu ya azimio la Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa wamepinga vikali azimio hilo lililopendekezwa na Marekani kupitia waraka huo.
-
Mchambuzi: Utawala wa sasa wa Syria utaifanya nchi igawanyike vipande vipande
Nov 17, 2025 07:19Mtafiti wa mahusiano ya kimataifa Yasser Al-Khatib amesema, hali ya mambo nchini Syria ni ngumu na tata mno kutokana na udhaifu wa watawala wake wa sasa, ambao unawasukuma watawala hao kutafuta msaada kutoka nje ya nchi, huku Wasyria wakighariki kwenye dimbwi la mgawanyiko wa nchi unaosababishwa na maslahi yanayokinzana ya nchi zinazoingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.