Waislamu Marekani wataka kudhaminiwa usalama
Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani (CAIR) limeitaka serikali ya nchi hiyo kuzidisha usalama na kulinda misikiti ya vituo vya Kiislamu husuan katika jimbo la New York.
Wito huo umetolewa baada ya kukithiri mashambulizi dhidi ya Waislamu na vituo vya Kiislamu nchini Marekani.
Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani (CAIR) ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi inayotetea haki za Waislamu nchini Marekani pamoja na Jumuiya ya Mawakili Waislamu wa Marekani zimelitaka Baraza la Mji wa New York kuchunguza kwa kina suala la mashambulizi yanayolenga Waislamu na vituo vya Kiislamu.
Awali CAIR pia iliitaka Idara ya Polisi ya New York kuchunguza sababu za chuki dhidi ya Waislamu baada ya Mwislamu mmoja kushambuliwa mje kidogo ya Msikiti wa Quins. Imam wa Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu cha New York pia alishambuliwa na Wamarekani wenye chuki na ubaguzi wa kidini siku chache zilizopita.
Ifaf Nashir ambaye ni Mkurugenzi Mtendeaji wa tawi la CAIR mjini New York amesema mashambulizi ya sasa dhidi ya misikiti nchini Marekani yanaonesha haja ya kuongezwa hatua za kiusalama na kuzidishwa idadi ya polisi kandokando ya maeneo ya Kiislamu.