Jan 14, 2024 07:39 UTC
  • Mkuu wa sera za kigeni wa EU: Ni muhimu kusitisha vita Gaza

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa ni muhimu kusitisha vita Ukanda wa Gaza. Josep Borrell ameeleza haya katika mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi za Asia Magharibi walipojadili matukio ya karibuni huko Palestina.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa Josep Borrell Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa kuna umuhimu sasa wa kusitishwa kile alichokitaja kuwa mapigano na kuachiwa huru mateka wote  kwa kuzingatia kuuliwa Wapalestina 24,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto na pia hali ya kibinadamu ya kusitisha inayowakabili zaidi ya watu milioni mbili wakazi wa Ukanda wa Gaza; ambapo hivi sasa karibu wote hao ni wakimbizi. 

Jinai za ukatili za Israel dhidi ya watoto wa Gaza 

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ameashiria mazungumzo aliyofanya na viongozi wa Lebanon na kuongeza kuwa: nchi hiyo inaendelea kuwapokea wakimbizi zaidi ya milioni mbili; na kwamba ni majukumu mazito licha ya misaada muhimu inayotolewa na Umoja wa Ulaya na ya taasizi zinazowahudumia wakimbizi. 

Tangu tarehe 7 mwezi  Oktoba mwaka jana utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi,  huku  jamii ya kimataifa na jumuiya za haki za binadamu zikinyamaza kimya mkabala wa jinai za Israel.  Kimya hicho cha jamii ya kimataifa kimeutia kiburi utawala haramu wa Israel kuendeleza mauaji yake ya kinyama dhidi ya wanawake na watoto wa Palestina. 

Tags