Polisi 4 wa Marekani wauawa Dallas, maelfu wapinga ukatili wa polisi
Maafisa 4 polisi ya Marekani wameuwa baada ya 11 miongoni mwao kupigwa risasi katika maandamano ya wananchi wanaopinga ukatili wa polisi ya nchi hiyo dhidi ya Wamarekani weusi katika mji wa Dallas, Texas.
Maandamano hayo yamefanyika kulaani mauaji ya Wamarekani wawili wenye asili ya Afrika ambao wamepigwa risasi na kuuawa na polisi katika majimbo ya Louisiana na Minnesota.
Inaaminika kuwa polisi hao walipigwa risasi na walenga shabaha wawili wakati wa maandamano ya wananchi waliokuwa wakilalamikia mauaji yanayoendelea kufanywa na polisi wazungu wa Marekani dhidi ya raia wenye asili ya Afrika.
Polisi ya Marekani inawashikilia washukiwa watatu wa mauaji hayo.
Maandamano ya jioni ya jana huko Dallas yalichochewa na kitendo cha polisi ya Marekani cha kumpiga risasi kadhaa Philando Castile Jumatano iliyopita na Alton Sterling, siku moja baadaye.
Maandamano ya Dallas ni sehemu ya maandamano kama hayo ya kupinga ukatili wa polisi ya Marekani yaliyofanyika jana katika miji kadhaa ya Marekani.