Mar 03, 2024 04:38 UTC
  • Bolivia yataka kufunguliwa mashtaka Netanyahu katika mahakama ya ICJ

Wizara ya Mambo ya Nje ya Bolivia ametoa wito wa kufunguliwa mashtaka Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Wizara ya Mambo ya Nje ya Bolivia imetangaza katika taarifa yake kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na washirika wake katika mahakama ya ICJ kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu.  

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Bolivia imelaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa vita katika eneo hilo haraka iwezekanavyo. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Bolivia pia imekosoa hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuzuia kuingizwa misaada ya kibinadamu Ukanda wa Gaza na kusema, hatua hiyo inakinzana na vifungu na masharti ya  Mkataba wa Geneva na amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliyoagiza kusimamishwa mashambulizi, kuachiwa huru mateka na kudhaminiwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza. 

Mwezi Oktoba mwaka jana Bolivia pia ilikata uhusiano wake na Israel ikilalamikia jinai zinazoendelea kufanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya Gaza.  

Mwezi uliopita pia serikali ya Nicaragua iliunga mkono kesi iliyowaslishwa ICJ na serikali ya Afrika Kusini dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.  

Hii ni katika hali ambayo, walimwengi wanaendelea kueleza hasira na upinzani wao dhidi ya mashambulizi na mauaji ya watu wasio na hatia huko Gaza huku nchi za Magharibi zikiendelea kuunga mkono utawala wa Kizayuni. 

Tags