Jul 11, 2016 16:57 UTC
  • Amnesty yaeleza wasiwasi kutokana na kukamatwa waandamanaji Marekani

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na kukamatwa waandamanaji wanopinga ukatili wa polisi nchini Marekani.

Amensty International imetangaza kuwa, idadi ya watu waliotiwa nguvuni katika maandamano hayo ya amani katika mji wa Baton Rouge inatia wasiwaasi. Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema kuwa, maafisa wa polisi hawapaswi kutumia misimamo ya kindumakuwili katika kutekeleza sheria wakati wa maandamano na kwamba jukumu lao ni kutayarisha mazingira mazuri ya kufanyika maandamano hayo.

Polisi ya Marekani imewatia nguvuni waandamanaji zaidi ya 160 wanaopinga ukatili wa polisi katika mji Baton Rouge. Maandamano hayo ambayo sasa yameenea katika miji mbalimbali ya Marekani yalianza baada ya polisi wazungu wa nchi hiyo kuwaua kwa kuwapiga risasi Warekani wawili wenye asili ya Afrika katika majimbo ya Louisiana na Minnesota.

Mauaji hayo yamezusha tena wasiwasi mkubwa kote duniani kuhusu ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya raia weusi wa nchi hiyo.

Tags