Mauaji ya Waislamu wa Srebrenica yakumbukwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11053-mauaji_ya_waislamu_wa_srebrenica_yakumbukwa
Maelfu ya watu leo wameshiriki katika shughuli ya kukumbuka maelfu ya Waislamu wa Srebrenica waliouawa kinyama na Waserbia wa Bosnia Herzegovina miaka kadhaa iliyopita.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 11, 2016 16:59 UTC
  • Mauaji ya Waislamu wa Srebrenica yakumbukwa

Maelfu ya watu leo wameshiriki katika shughuli ya kukumbuka maelfu ya Waislamu wa Srebrenica waliouawa kinyama na Waserbia wa Bosnia Herzegovina miaka kadhaa iliyopita.

Maelfu wa Wabosnia walioshiriki katika shughuli hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Potocari kandokando ya mji huo wamelaani mauaji hayo na kuwakumbuka ndugu zao waliouawa kinyama na Waserbia.

Takwimu zinaonesha kuwa, Waislamu wasiopungua elfu nane waliuawa kwa umati wakati Waserbia waliposhambulia mji wa Srebrenica uliokuwa chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa. Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilitangaza kuwa Radovan Karadzic aliyekuwa kiongozi wa Waserbia wa Bosnia ndiye aliyehusika na kitendo cha kuzingirwa mji wa Sarayevo na jinai zilizofanyika katika miji na vijiji vingine ya Bosnia Herzegovina katika vita vya Bosnia kwenye muango wa 1990.

Katikati ya mwezi Julai mwaka 1995, majeshi ya Serbia yakiongozwa na Jenerali Ratco Mladic yaliwauwa kwa halaiki Waislamu wanaokaribia 8,000 wa Srebrenica wakiwemo wanawake na watoto, na mauaji hayo kunahesabiwa kuwa makubwa zaidi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia.