Jul 13, 2016 15:20 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu ongezeko la HIV

Idara ya Kupambana na Virusi vya HIV ya Umoja wa Mataifa (UNAIDS) imetahadharisha kuhusu ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo kote duniani baada ya kuripotiwa habari za kuongezeka kesi za mambuzi ya virusi hivyo hatari.

UNAIDS imetahadharisha kwamba mwenendo wa kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya HIV unakwenda taratibu sana kote duniani na kutangaza kuwa, uchunguzi mpya unaonesha kwamba, maambukizi ya virusi hivyo baina ya watoto yamepungua kwa asilimia 70 tangu mwaka 2001 lakini maambukizi yake bina ya watu wazima yanaongezeka.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé, amesema uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika baadhi ya maeneo umefika kiwango cha sifuri na kwamba iwapo maeneo hayo yatakumbwa tena na virusi hivyo kutashuhudiwa maambukizi makubwa ambayo hayawezi kudhibitiwa.

Takwimu za UNAIDS zinaonesha kuwa, katika kipindi cha miaka 5 iliyopita karibu watu milioni moja na laki tisa huambukizwa virusi vya Ukimwi kila mwaka.

Tags