Papa: Inaungulisha nyoyo kuona sheria za kimataifa haziheshimiwi tena
(last modified Sat, 28 Jun 2025 08:41:59 GMT )
Jun 28, 2025 08:41 UTC
  • Papa Leo
    Papa Leo

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo amesema, inaungulisha nyoyo kuona sheria za kimataifa haziheshimiwi tena.

Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X, kiongozi huyo wa kidini amesema: “inaungulisha nyoyo kuona leo hii nguvu za sheria za kimataifa na sheria za masuala ya kibinadamu haiheshimiwi tena, kwa mahala pake kuchukuliwa na kinachoonekana kuwa ni haki ya kujipa nguvu na mamlaka juu ya wengine”.

“Hili ni jambo lisilolaiki na la kuaibisha kwa ubinadamu na kwa viongozi wa mataifa”, ameongezea kusema Papa Leo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amekumbusha pia kuwa historia imethibitisha kwamba vita huwa havileti amani.

Amehoji: “tunawezaje kuamini, baada ya karne kadhaa za historia, kwamba hatua za kivita zinaleta amani na si kuwageukia wale wanaoanzisha?”

Papa Leo amesisitiza kuwa, misingi ya kesho inapasa ijengwe kwa mshikamano na kwa maono ya pamoja yanayohamasishwa na matendo mema ya wanadamu wote…/